Friday, October 30, 2020

KAGERE: ETI MAKAMBO? MSINITANIE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SAADA SALIM


 

WAKATI baadhi ya mashabiki wa Yanga wakisema Meddie Kagere wa Simba ni ‘chamtoto’ kwa Heritier Makambo, Mnyarwanda huyo amekuja juu akitaka kutofananishwa na mchezaji yeyote, kwani anajua nini anakifanya.

Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakitambia ubora wa Makambo, wakidai kuwa usajili wa straika huyo ni ‘bab kubwa’, huku wakimponda Kagere kwa madai kuwa umri wake utamsababisha kushindwa kufanya vizuri na kwamba Simba wameingizwa mkenge kumsajili straika huyo kutoka Rwanda.

Jeuri ya Yanga inatokana na Makambo kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akifunga moja, kitu ambacho kinawafanya Wanajangwani hao kudai kuwa Kagere atasubiri sana.

Akijibu mapigo ya mashabiki hao, Kagere alisema amekuja kikazi zaidi na mpango wake ni kuhakikisha Simba wanatwaa mataji mbalimbali, hivyo wanaomfananisha na mchezaji mwingine wanajisumbua bure.

“Mimi siwezi kujizungumzia mwenyewe, mafanikio ya Simba ni yetu Wanasimba wote, ninachokiangalia ni kupambana kuhakikisha timu kwa ujumla inafanya vizuri na kutwaa makombe, hivyo nisifananishwe na huyo straika wa Yanga (Makambo) wala mwingine yeyote,” alisema.

Alisema anafurahi mno kwa jinsi mashabiki wao wanavyoiunga mkono timu yao na kuahidi kwamba atashirikiana na wachezaji wenzake kuhakikisha wanatetea ubingwa wao na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Kagere, aliyetua Simba msimu huu, tayari ameshaisaidia timu hiyo kubeba Ngao ya Jamii, walipoifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba wiki iliyopita, huku straika huyo akifunga bao la kwanza.

Nyota huyo aliendeleza cheche zake katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons alipofunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano ya wiki hii.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -