Sunday, October 25, 2020

YOUNG STINO KIPAJI KIPYA BONGO FLEVA ALIYEAPA KUMPOTEZA MSAMI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA GLORY MLAY


WASANII wa muziki wa hip hop siku zote wanafahamika kwa kutokata tamaa, wakipenda kusimamia kile wanachokiamini bila kujali changamoto wanazokutana nazo.

Mara nyingi, nyimbo za wanamuziki wa aina hiyo zimekuwa zikiigusa jamii moja kwa moja, huku zikienda sambamba na matukio yaliyopo kwa wakati huo, hali inayowafanya wapate mashabiki wengi na rika zote.

Wasanii kama Roma Mkatoliki na Ney wa Mitego, hivi sasa wamewateka mashabiki wa aina mbalimbali kutokana na mashairi ya baadhi ya nyimbo zao kugusa maisha ya watu wengi.

Licha ya kwamba kuna baadhi ya nyimbo zao zinawaingiza katika matatizo, lakini wameendelea kuwa na msimamo kwa kuhakikisha wanachokifanya kinakwenda sawa na malengo waliyojiwekea.

Stephano Arnold ‘Young Stino’, naye ni msanii chipukizi wa muziki huo wa hip hop, ambaye naye amekumbana na misukosuko hadi kufika aliposasa.

Msanii huyo kwa sasa anatamba na wimbo wake unaoitwa Wale Wale ambao amemshirikisha msanii wa Bongo Fleva aliyemtaja kwa jina la Paulina Mukoba, maarufu kama P na umeanza kufanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini.

Wiki iliyopita, BINGWA lilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Young Stino kuhusiana na suala zima la ngoma yake mpya na mambo mengine mengi.

BINGWA: Wale Wale ni wimbo wako wa ngapi?

Stino: Ni ngoma yangu ya nne kutokana na ‘ku-hit’, nimefanya kazi nyingi lakini watayarishaji wengi wameniambia hazina viwango, hivyo nimeamua kuanza upya.

Ngoma yangu ya kwanza inaitwa Shikamoo Pesa ya pili Changamoto niliyomshirikisha Mr. Blue, Dalali niliyoimba na Barnaba na hii ya sasa ya Wale Wale ambayo nimeimba na Paulina anayejulikana kwa jina la P.

BINGWA: Kwanini uliamua kumshirikisha P katika kazi yako ya Wale Wale?

Stino: Msanii huyo anajitahidi katika kazi yake, lakini bado hafanikiwa kutoka, hivyo kitendo cha kumshirikisha kinampa nafasi ya kujulikana katika jamii.

Ni njia mojawapo ya kumwinua ili naye awe miongoni, mwa akina dada wanaochipukia katika muziki huu wa Bongo Fleva.

BINGWA: Ngoma hiyo imefanyiwa wapi?

Stino: Nimeufanya katika studio za Star J na mtayarishaji akiwa ni Star J, akishirikiana na mwongozaji Ton Brause na wimbo huu upi katika mahadhi ya Bongo Fleva.

BINGWA: Ngoma hiyo ya Wale Wale ni kisa cha kweli au umeimba tu kama wimbo wa kawaida?
Stino: Yap, ni kisa ambacho kilinitokea mimi ambapo mpenzi wangu alikuwa anasikiliza maneno ya watu wa pembeni wanasema nini juu yetu. Matokeo yake Msami alinipokonya tonge mdomoni.

BINGWA: Je, una mpango wa kulipiza kisasi kwa Msami?
Stoni: Ndio, nitalipiza ila kisasi changu nataka kumfunika kimuziki, nahitaji kufanya kila njia ili niweze kumzidi kwa kuwa najua hajui kuimba, ila watayarishaji wanampa sifa kutokana na umaarufu alionao.

Mimi sitaangalia umaarufu wake bali kumzima kimuziki asiweze kusikika, nataka kuwa wa kimataifa.

BINGWA: Je, kwa sasa una uongozi unaosimamia kazi zako?
Stino: Hapana, bado sijapata uongozi wowote, nahitaji kupata uongozi ambao utanisimamia katika kazi yangu hii lakini si WCB (Wasafi Classic Baby).

Nikiwa na uongozi naamini kila kitu kitakwenda sawa, hivyo naomba mtu yeyote aliye tayari kunisimamia basi nitakunjua mikono yangu kumpokea.

BINGWA: Kwanini haupo tayari kusimamiwa na WCB?
Stino: Hapana, sitakubali kusimamiwa na uongozi huo. Nimesikia ukiingia katika kundi hilo, kazi zako kwanza hazitaonekana na hata ukitoa kazi, faida yote inachukuliwa na wao, unajikuta mwisho wa siku huna chochote, kwa hiyo maisha yangu yote sitaweza kufanya nao kazi.

BINGWA: Ahsante sana kwa ushirikiano wako, tunakutakia kila la heri katika safari yako ya muziki.

Young Stino: Ahsante sana nami nakushukuru kwa kunipa nafasi katika magazeti yenu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -