Friday, October 23, 2020

TFF YAMFUNGIA MBASHA MATUTU MAISHA  

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA LULU RINGO


KAMATI ya  maadili ya shirikisho la  soka Tanzania (TFF, ) imemfungia maisha  msimamizi wa kituo cha Shinyanga na mjumbe wa TFF mkoani humo,  Mbasha Matutu asijihusishe na masuala ya soka baada ya kupatikana  na hatia ya upotevu wa fedha Sh milioni 16.

Fedha hizo zilipotea katika msimu uliopita wa  Ligi Kuu Tanzania Bara, kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza kati ya Simba dhidi ya Stand United iliyochezwa katika Uwanja wa Kambarage Shinyanga, ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, na kuingiza mapato ya Sh milioni 36.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti  wa kamati ya maadili, Hamid Mbwezeleni,  amesema Matutu alituhumiwa kwa makosa matatu ambayo baada ya uchunguzi ilibainika kuwa na hatia hali ambayo ilifanya uongozi kumsimamisha kabla ya kumfungia ili kupisha uchunguzi.

Mbwezeleni aliyataja makosa hayo ni kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kazi kama mkuu wa kituo, ubadhirifu wa fedha pamoja na kugushi na kuiba ambapo baada ya uchunguzi kukamiliaka alibainika kuhusika kwa tuhuma hizo.

Alisema katika mchezo huo Matutu alikabidhiwa vitabu 70 vya kukatia risiti vikauzwa vyote kwa bei ya Sh. 5000 kwa watazamaji 700 walioingia uwanjani hapo lakini mapato yaliyowasilishwa ni pungufu.

“Kabla ya kufungiwa Matutu alipewa nafasi ya kujitetea kutokana na tuhuma zilizomkabili, lakini alishindwa kutoa utetezi unaoeleweka hali ambayo ameonekana na  hatia,” amesema mwenyekiti huyo  .

Mbwezeleni, amesema wamemfungia kwa kuzingatia vifungu vya sheria ikiwemo ubadilifu, kugushi ma kuiba kinyume na kanuni ya 13 (4), kanuni ya 73 (7) cha kanuni ya ligi kuu ya 27, kushindwa kutekeleza  majukumu yake kama msimamizi wa kituo kinyume cha kifungu 41(19) cha kanuni za ligi kuu toleo la mwaka  2013.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -