Wednesday, October 21, 2020

TSHISHIMBI, KAMUSOKO WAJIENGUA YANGA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA SAADA SALIM


NYOTA wawili wa Yanga, Papy Tshishimbi na Thaban Kamusoko hawatakuwamo katika kikosi kilichoondoka jana saa 7:00  usiku kwenda Rwanda kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports utakochezwa kesho.

Yanga iilitarajiwa kuondoka jana usiku kuelekea nchini humo, huku ikiwakosa nyota wake hao muhimu kwa madai ya kuwa majeruhi.

Lakini taarifa za ilizozipata BINGWA jana, ni kwamba wachezaji hao hawakuwa na mpango wa kuondoka na timu kutokana na madai ya kutolipwa mishahara yao na hawakushiriki katika mazoezi ya jana asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.

“Tshishimbi, Kamusomo, wamemweleza kocha kwamba wanaumwa hivyo hawatakwenda katika safari hiyo, lakini ukweli ni kwamba wachezaji hao wamejitoa katika safari kutokana na madai yao ya mishahara,” alisema.

BINGWA lilimtafuta Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera alithibitisha kuwa watawakosa wachezaji hao wawili pamoja na Haji Mwinyi, Amis Tambwe, Said Makapu, Juma Abdul na Juma mahadhi kutokana na sababu mbalimbali.

Alisema anachofahamu kwa Tshishimbi na Kamusoko ni suala la kifedha licha ya kuficha, kwani hana taarifa za kidaktari kwamba wanaumwa licha wao wanasema wanajisikia vibaya na kushindwa kwenda Rwanda.

“Tumemaliza mazoezi yetu ya asubuhi ikiwa ni mandalizi ya mwisho kuelekea Rwanda, lakini nyota hao hawatakuwepo wengine wanamatatizo ya kifamilia na majeruhi.

“Tshishimbi na Kamusoko sijui matatizo yao, unajua tatizo la wachezaji wengi shida kubwa ni mishahara yao, sasa kila mtu anasema anaumwa.”

Alisema licha ya baadhi ya wachezaji wake kutokuwepo wana imani watafanya vema kama ilivyokuwa mchezo uliopita wa michuano hiyo dhidi ya USM Alger kwa kushinda mabao 2-1.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -