Wednesday, October 28, 2020

NIMEUELEWA USHIRIKI WA WASANII KATIKA TAMASHA LA URITHI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA CHRISTOPHER MSEKENA


KUELEKEA tamasha la urithi litakaloanza kufanyika Septemba 1 mpaka 29 mwaka huu sehemu mbalimbali nchini, uwepo wa wasanii wa muziki na sanaa zingine katika tukio hilo lililoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii limetuvutia wengi.

Wasanii wameendelea kupata nafasi ya kushiriki katika matukio makubwa na muhimu ya nchi, ikiwa ni ishara ya heshima ambayo sekta ya sanaa inajipatia kutokana na kazi zao zinazoonekana mbele ya viongozi na wakuu wa nchi.

Kwa maana hiyo halitakiwa jambo la ajabu tena wasanii kushiriki katika miradi mkubwa ya serikali, kwa kutumia nafasi zao kwenye jamii kama wasanii na vioo vinavyo tazamwa na wengi kufikisha jumbe mbalimbali zinazokusudiwa.

Kama tunavyojua muziki au sanaaa kwa ujumla ndiyo kitu pekee kinachoweza kumfikia mtu na kumpa elimu ya jambo fulani bila bugdha yoyote na akaitumia hiyo elimu kujiletea mabadiliko chanya mwenyewe kwenye maisha yake.

Hivyo basi ushiriki wa wasanii mbalimbali katika tamasha la urithi, ni mpango ambao nimeuelewa kwa sababu lengo kubwa ni kuhakikisha jamii inakumbuka kule ilikotoka na urithi ambao tunao kama nchi.

Tayari mastaa wa muziki nchini kama vile Jux, Joel Lwaga, Joh Makini, Nikki wa Pili, G Nako, Ditto, Nandy, Mario, Mrisho Mpoto, Mimi Mars, Vanessa Mdee,Bright, Amin, Mwasiti, Jay Melody na wengine wengi wameingia studio za Epic Records kuandaa wimbo wa tamasha hilo maarufu kama Kachumbali La Urithi.

Tamasha  hilo ambalo linatarajia kupita katika mikoa kadhaa Tanzania kama vile, Dodoma (Uwanja wa Jamuhuri), Zanzibar (Stone Town na Mapinduzi Square), Dar es Salaam (Manazi Mmoja), Mwanza (Furahisha), Karatu (Viwanja vya Mazingirabora) na Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume limedhamiria kuikumbusha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya urithi wetu kama Tanzania.

Kupitia sanaa na matukio mengine yatakayofanyika katika matamasha hayo malengo yatakwenda kutimia kwani kuanzia mavazi, chakula, maliasili, vitutio na vingi vya kuiuza nchi yetu duniani vitakwenda kuongezewa mkazo mbele ya jamii.

Tamasha la urithi limejiwekea malengo ya kutangaza utambulisho wa mtanzania, alama za Taifa, umoja na mshikamano wetu. Kutanzania utajiri wa  mbuga, milima na vingine ambavyo Mungu ametujalia.

Hali kadharika tamasha hilo limelenga kuongeza thamani ya asili ya mtanzania, kutangaza vivutio vyetu ambavyo vinapatikana Tanzania pekee na siyo nchi nyingine duniani.

Kupitia  ushirikiano wa wasanii katika tamasha hili, bila shaka ujumbe ambao umekusudiwa utafika mahala pake, jamii itaelewa thamani ya urithi wetu, itaulinda na kuutangaza kadri inavyowezekana.

Binafsi nimeuelewa mchanganyo huu wa sanaa na masuala ya urithi wetu kama Taifa, hatupaswi kuishia hapa, sanaa yetu ndiyo kwanza imechanua hivyo ushirikaiano wa wasanii na Wizara mbalimbali katika kunadi urithi wetu ni muhimu.

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -