Tuesday, October 20, 2020

FEI TOTO: MLETENI HUYO MKUDE WENU

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

 

NA SALMA MPELI


 

KIUNGO machachari wa Yanga, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’, amesema kuwa yupo tayari kukutana na Jonas Mkude wa Simba pamoja na umahiri wa nyota huyo wa watani wao wa jadi anayeaminika kuwa kiungo mkabaji bora kabisa hapa nchini.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Septemba 30, mwaka huu katika mchezo wa kwanza baina ya wakongwe hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku mashabiki wa timu yake wakionekana kujivunia naye mno kutokana na kiwango alichokionyesha katika mechi mbalimbali.

Katika mechi alizocheza, Fei Toto, ikiwamo ya kirafiki dhidi ya Mawenzi Market kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na wa Ligi Kuu Bara walipoivaa Mtibwa Sugar wiki iliyopita, Mzanzibari huyo alicheza vizuri mno kiasi cha kuwafanya mashabiki wa Yanga kutamani kumwona nyota wao huyo akipimana ubavu na Mkude.

Alipoulizwa juu ya hilo mwishoni mwa wiki iliyopita, Fei Toto, alisema anamfahamu vizuri Mkude, ikiwamo uwezo wake uwanjani, akiamini kila mmoja ana kiwango chake.

Alisema amecheza dhidi ya timu nyingi za Tanzania Bara wakati akiwa na kikosi cha JKU ya Zanzibar, hivyo mashabiki ndio wanaweza kupima na kuwalinganisha uwezo wao.

“Naamini Mkude ana uwezo wake na mimi ninao wangu pia, hanizidi kwa kiasi kikubwa ni kama tunalingana tu, nadhani tutakapokutana, mashabiki wataweza kutupima,” alisema.

Akilizungumzia pambano la watani wa jadi hao, Fei Toto, alisema mchezo baina ya timu hizo ni kama ilivyo mingine, hivyo analichukulia la kawaida tu, huku akiamini kikosi chao chini ya Kocha Mkuu wao, Mwinyi Zahera, kitafanya vizuri na hatimaye kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

“Naamini tuna timu nzuri na kulingana na maandalizi yetu yanavyokwenda sawa, Mungu akinijalia nitafanya vizuri kuisaidia timu yangu kutwaa ubingwa. Kama ni hao Simba, ni wa kawaida kwani nimeshakutana nao sana nikiwa na JKU katika mashindano ya Cecafa na SportPesa,” aliongeza Feisal.

Yanga wameshacheza mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kushinda mabao 2-1.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -