Wednesday, October 28, 2020

TWANGA PEPETA KUADHIMISHA MIAKA 20

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU


 

BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, The African Stars ‘Twanga Pepeta’, imeanza maaandalizi ya kufanya onyesho kubwa la kuadhimisha miaka 20 toka kuanzishwa kwake mwaka 1998.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, ameliambia Papaso la Burudani kuwa onyesho hilo litafanyika katika ukumbi wa Club Legends uliopo Namanga jijini Dar es Salaam na shughuli kama kutembelea vyombo vya habari, kusaidia watoto yatima na wagonjwa zitafanywa na wanamuziki wa Twanga Pepeta.

“Miaka 20 si midogo kudumu katika shughuli za muziki, kwa kweli tumepitia changamoto nyingi sana, wanamuziki kuhama, soko la muziki wa dansi kushuka kutokana na mabadiliko ya sekta hiyo ikiwamo kuibuka kwa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva), Taarab na Singeli, tulifanikiwa kuzindua albamu 14, mashabiki walibadili mwelekeo lakini sasa mambo yamerejea,” alisema Baraka.

Aliongeza kuwa ndani ya miaka hiyo, Twanga Pepeta chini ya Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (Asets), wameweza kupata mafanikio mengi ikiwa ni pamoja na kuzindua albamu 14, kuasisi bendi nyingine kama African Revolution enzi ya Chumvi Chumvi, Tam Tam mpaka Vibration Sound huku ikifanya maonyesho makubwa ndani na nje ya nchi kama Norway, Sweden, Denmark, Finland, Uingereza na Oman pamoja na kuibua vipaji lukuki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -