Monday, October 26, 2020

DE GEA ASISITIZA MAN UTD HAITAANGUKA KAMWE

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

MANCHESTER, England


 

SAA chache tangu ziibuke taarifa za wachezaji na wafanyakazi wa klabu ya Man Utd kuwa na imani kwamba kocha, Jose Mourinho, huenda akatimuliwa iwapo timu hiyo itafungwa na Burnley wikiendi hii, David De Gea  anafikiri tofauti.

Mlinda mlango huyo ambaye kwa sasa ana wakati mgumu katika kikosi hicho akishindwa kukisaidia kuepukana na vipigo vya aibu, amesema Man Utd imeungana na wapo imara zaidi.

Tangu United ilipokubali vichapo dhidi ya Brighton na Spurs, wengi wamekuwa na mtazamo kwamba bosi wa United, Ed Woodward, atamtimua Mourinho.

Aidha, baadhi ya wachezaji wa United wamekuwa wakilitaja jina la Zinedine Zidane kuwa ndiye atakuwa kocha wao baada ya Mourinho kufukuzwa.

Hali hiyo pia iliwahi kumkuta Louis van Gaal katika siku zake za mwisho mwaka 2016 kabla nafasi yake haijachukuliwa na Mourinho.

Chanzo cha habari kiliutonya mtandao wa Daily Mail kwamba: “Kuna baadhi ya wachezaji wanasema Mourinho ataondoka hivi karibuni. Wengine wanahisi wakipoteza tena kwa Burnley  ndio basi. Na wengine hawaoni kama atadumu hadi Septemba.”

“Hata kama United wanasema wapo nyuma ya Mourinho, walishasema hivyo kwa Van Gaal lakini mwisho wake tuliuona. Wachezaji wameanza kumtaja Zidane wakati Mourinho bado hajaondoka,” kiliongeza chanzo hicho.

Juzi klabu hiyo ilitoa kauli kwamba itaendelea kushirikiana na Mourinho na kuna nafasi finyu ya Mreno huyo kuondoka kwani bado ana mkataba wa mwaka mmoja.

Baada ya kauli hiyo, De Gea akitumia mtandao wa kijamii, naye alisisitiza kwamba timu nzima imeungana pamoja katika nyakati hizi ngumu.

Jana kulikuwepo na ripoti zilizodai kwamba, Mourinho amebakiza mechi moja kabla ya kufungashiwa virago vyake, hasa baada ya kuibuka kwa taarifa za wachezaji kumuota Zidane kuwa kocha wao wa baadaye.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -