Tuesday, October 27, 2020

KAKA ANA BAO MOJA TU KWENYE KOMBE LA DUNIA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

KATIKA miaka ya hivi karibuni, majina ya wachezaji kadhaa wa Kibrazil yameweza kutamba kwenye soka, hasa katika masuala ya usajili.

Wachache kati yao ni pamoja na Neymar, aliyetua PSG kwa ada iliyoweka rekodi, sawa na Coutinho, ambaye alisajiliwa na Barcelona kwa uhamisho uliotikisa dunia.

Nyota hao wamefuata nyayo za waliowatangulia na mmoja wa wachezaji hao wa zamani wa Brazil ambao walitisha sana enzi zao ni Kaka. Yafuatayo ni mambo 10 usiyoyafahamu kumhusu kiungo huyo wa zamani wa Sao Paulo, AC Milan, Real Madrid na Chicago Fire FC.

1. Jina lake halisi ni Ricardo Izecson dos Santos Leite. Lakini anajulikana sana kama Ricardo Kaka, kwa sababu kaka yake alishindwa kutamka ‘Ricardo’ alipokuwa mdogo na alianza kumuita Caca. Jina lililodumu hadi leo.

2. Kama si soka, Kaka angecheza tenisi kabla ya kuachana na mchezo huo alipokuwa mdogo. Haukuwa uamuzi mbaya sana kwake, kwani alikutana na mafanikio makubwa mno alipoamua kusakata kandanda.

3. Huenda pia Kaka asingeendelea na soka kwa muda mrefu kama si matibabu mazuri aliyopata baada ya kuumia uti wa mgongo alipoteleza kwenye bwawa la kuogelea. Ni muujiza uliofanikisha kupona kwake.

4. Licha ya taifa la Brazil kutawaliwa na changamoto ya umasikini mkubwa, lakini Kaka alitokea katika familia tajiri. Alinolewa vyema katika soka na msingi wa maisha yake bora ya soka ulianza vizuri.

5. Kaka ndiye mchezaji pekee duniani aliyempa wakati mgumu Lionel Messi katika mechi ya kirafiki kati ya Brazil na Argentina, ambapo Kaka alifunga bao tamu baada ya kumzidi mbio Messi kutoka katikati ya uwanja.

6. Pia gwiji huyo anahusika na masuala kadhaa ya hisani. Mbrazil huyo ni balozi wa Programu ya Chakula Duniani chini ya Umoja wa Kimataifa (UN). Pia ni balozi wa michezo maalumu ya Olimpiki.

7. Kiungo huyo ni mmoja wa wachezaji nane walioweza kunyakua Kombe la Dunia, taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d’Or.

8. Licha ya kusifika kuwa na kasi, uwezo wa kung’amua nafasi za mabao na mashuti ya mbali, Kaka hajawahi kumaliza msimu na zaidi ya mabao 20. Aliyofunga mengi ni 23 mwaka 2002 akiwa Sao Paulo.

9. Kaka ana bao moja tu katika michuano ya Kombe la Dunia, alilifunga mwaka 2006 dhidi ya Croatia. Mwaka 2010 alitarajiwa kuonesha tena uwezo wake, lakini alilimwa kadi nyekundu dhidi ya Ivory Coast.

10. Pia ni mwanamichezo wa kwanza kufikisha mashabiki milioni 10 katika mtandao wa kijamii wa Twitter. Kwa sasa ana mashabiki milioni 29.6.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -