Tuesday, October 27, 2020

BIASHARA WAJIONDOA MBIO ZA UBINGWA TPL

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA


SIKU moja baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United, Kocha Msaidizi wa Biashara, Amani Josiah, amesema msimu huu hawahitaji ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara zaidi ya kujitengenezea mazingira mazuri kwenye michuano hiyo.

Biashara ambayo ni miongoni mwa timu sita zilizofanikiwa kupanda Ligi Kuu Bara msimu huu, mpaka sasa imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo mitatu iliyocheza mpaka sasa.

Akizungumzia mipango ya timu hiyo, Josiah alisema Biashara ni timu mpya kwenye ligi, hivyo mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kuwa na uvumilivu, kwani kwa mwaka huu hawana nia ya kutwaa ubingwa.

“Hii ni timu mpya, watu wanapaswa kuwa wavumilivu halafu hatuwezi kuwepo kwenye mbio za ubingwa kwa kuwa tunapaswa kujijenga zaidi na kuwa imara,” alisema.

Alisema kwa kipindi hiki mashabiki wawe tayari na matokeo yote matatu ya kufungwa, kushinda na sare, kwani kikosi chao bado hakijaweza mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara.

“Tumefungwa jana lakini wapinzani wetu walitumia udhaifu wetu kidogo tu, mpira una matokeo matatu watu wawe na uvumilivu,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -