Wednesday, October 28, 2020

YANGA WAZIDI KUSHANGAZA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...


*Wanayoyafanya wachezaji, hakuna anayeweza kuamini

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR

WACHEZAJI wa Yanga wameendelea kuwashangaza wapenzi wa soka nchini kutokana na uamuzi wao wa kuweka pembeni matatizo ya kiuchumi yanayowakabili na badala yake, kujifua vilivyo ili kuibeba timu yao katika mechi zao zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga imekuwa na utamaduni wa wachezaji wao kutoyumba pale klabu hiyo inapokabiliwa na hali mbaya kiuchumi au migogoro ya uongozi tofauti na ilivyo kwa Simba.

Mathalani, kuanzia msimu wa 2011/12, klabu ya Simba ilikuwa ikiandamwa na migogoro ya kiuongozi hali iliyowakimbiza wadhamini na wahisani mbalimbali na matokeo yake, kikosi chao kikawa wasindikizaji Ligi Kuu Bara, huku Yanga na Azam FC wakipishana kwenye nafasi mbili za juu.

Lakini mara baada ya klabu hiyo kuwa chini ya Kaimu Rais, Salim Abdallah ‘Try Again’ ambaye anaonekana wazi kusimama imara na kuiongoza klabu kwa kufuata taratibu na kanuni, mambo yamekuwa ‘muswano’ ndani ya Msimbazi kiasi cha msimu uliopita kutwaa ubingwa wa Bara.

Kama ilivyokuwa msimu uliopita, safari hii pia mambo yanaonekana kutokaa sawa Jangwani kiasi kwamba wachezaji wanadaiwa kutolipwa mishahara ya miezi mitatu.

Lakini pamoja na hilo, wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakipambana vilivyo katika mechi mbalimbali walizocheza ukitoa zile ambazo kikosi chao kilikuwa kikiandamwa na wimbi la majeruhi.

Katika kuonyesha jinsi wanavyoheshimu na kuuenzi utamaduni wa klabu yao, wachezaji wa Yanga wameendelea kujifua kwa nguvu zao zote katika mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, Dar es Salaam.

Jambo la kufurahisha zaidi kwa wachezaji hao, pamoja na kuwa chini ya kocha msaidizi, Noel Mwandila kwa kuwa Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera anaitumikia timu ya Taifa ya nchi yake ya DR Congo, akiwa kama kocha msaidizi, hilo limekuwa si tatizo kwa vijana wa Jangwani kujipanga hasa kuendelea kuuwasha moto Ligi Kuu Bara.

Yanga hadi sasa wamecheza mechi moja tu ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar na kushinda mabao 2-1, huku wakitarajiwa kushuka dimbani tena kuanzia Septemba 16, mwaka huu dhidi ya Stand United na Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ili kuhakikisha wachezaji wao wanakuwa fiti zaidi, Mwandila juzi na jana aliwahenyesha mno wachezaji wake kwa kuwapigisha tizi la kufa mtu ili kuwajengea stamina na pumzi ya kutosha kupambana kwa dakika zote 90 na hata zaidi.

Wachezaji wote waliohudhuria mazoezini walikuwa wakimpa kocha huyo ushirikiano wa hali ya juu, wakifuata na kuyatekeleza vilivyo maelekezo waliyokuwa wakipewa.

Akizungumzia mazoezi hayo, Mwandila alisema yanalenga kuiandaa Yanga mpya ambayo ni kwa ajili ya kusaka pointi tatu kila mechi zitakazowafanya wawe na uhakika wa kufanya vema msimu huu.

“Nakiandaa kikosi chetu kwa kila hali, lakini pia nimegawa majukumu kwa kila mchezaji atakayeingia uwanjani ahakikishe tunapata ushindi wa pointi tatu muhimu,” alisema.

Baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga kwa sasa akili zao zote wamezielekeza Ligi Kuu Bara ili waweze kulirejesha kombe lao waliloporwa na Simba msimu uliopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -