Tuesday, October 27, 2020

MOURINHO AMRUKA KIMANGA RONALDO

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

LONDON, England


KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, amezikana taarifa zilizosambaa zikieleza kwamba ndiye aliyeuambia uongozi wa klabu hiyo usimsajili straika wa zamani wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, wakati wa  dirisha la usajili majira haya ya joto.

Kabla ya kwenda kujiunga na Juventus kwa ada ya pauni milioni 90, Ronaldo alishafunga mabao 450 katika michezo  438 aliyoichezea klabu hiyo ya Real Madrid na katika kipindi hicho alichokuwa Bernabeu, Mreno huyo alikuwa akihusishwa kurejea Man  United, baada ya kujijengea jina tangu alipotua Old Trafford akitokea Sporting Lisbon.

Mbali na hilo akiwa na mashetani hao wekundu ndani ya kipindi cha miaka sita, Ronaldo, aliweza kufunga mabao 118 na mpaka sasa bado anakumbukwa na mashabiki wa klabu hiyo.

Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita ziliibuka taarifa zikieleza kwamba,  wakati wa usajili wa majira haya ya joto,  Mourinho, ndiye aliyeiambia Bodi ya Wakurugenzi wa Man Utd kuachana na Mourinho, lakini jana kocha huyo naye akazijibu akisema hakuwahi kuwa na ofa yoyote mezani kwake ya kumtaka straika huyo.

“Jina la Cristiano halijawahi kuja mezani kwangu ili niweze kusema ndio au hapana,” Mourinho aliwaambia waandishi wa habari.

“Ili Cristiano aje kwetu nasema wazi haijawahi kufika mezani kwangu,” alisisitiza Mreno huyo.

Juzi Man United walionekana kurejea katika njia ya ushindi katika michuano ya Ligi Kuu England, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya Burnley, baada ya kuanza kwa kusuasua na kujikuta wakipokea vipigo viwili mfululizo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -