Friday, October 23, 2020

SIMBA NI HATARI TUPU!

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

 

 

  • Kwa mazoezi anayotoa Mbelgiji, Sept 30 kuna watu watasahau makwao

WINFRIDA MTOI NA AYOUB HINJO


SIMBA ni hatari tupu! Hutakosea ukisema hivyo kutokana na kile kinachoendelea katika mazoezi ya timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems, raia wa Ubelgiji.

Pamoja na kuwa na safu hatari ya ushambuliaji, Aussems ameonekana kutoridhishwa na kasi ya mabao waliyovuna hadi sasa katika mechi zao mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara na hivyo kuendelea ‘kuwapika’ zaidi mastraika wake.

Katika mechi zao hizo za kwanza, Simba wamefunga mabao matatu, huku nyavu zao zikiwa hazijatikiswa na timu yoyote.

Akionekana mwenye kiu ya kuvuna mabao mengi zaidi kila mechi, Aussems jana aliendelea kuwanoa washambuliaji wake kuhakikisha wanatikisa zaidi nyavu za wapinzani wao.

Katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterans, Dar es Salaam jana jioni, Mbelgiji huyo alikuwa akiwafundisha washambuliaji wake mbinu mbalimbali za kufunga mabao, lakini pia kuwatoka mabeki.

Aliwataka vijana wake kutokubali kupoteza nafasi ya kufunga mabao kirahisi, lakini pia akiwajengea stamina ya kuwawezesha kupambana na mabeki, kuanzia katika kuwania mipira ya chini hadi ya juu.

Kocha huyo baada ya kuwapa vijana wake mazoezi ya stamina, aliunda vikosi viwili, cha kwanza kikiwa na washambuliaji John Bocco na Hassan Dilunga, huku nyuma yao wakiwamo Jonas Mkude na Mohammed Ibrahim.

Kikosi cha pili kilikuwa na washambuliaji Adam Salamba na Mohammed Rashid ambao walikuwa wakizungukwa na viungo, Shiza Kichuya na Said Ndemla.

Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha anakuwa na kikosi kipana ambapo hata ikitokea mshambuliaji fulani amekosekana, bado anakuwa na mbadala wa kuziba nafasi yake barabara.

Ikumbukwe kuwa mbali ya washambuliaji hao, Simba ina mastraika wakali kama Emmanuel Okwi, anayeitumikia timu yake ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ na Meddie Kagere aliyepo na kikosi cha Taifa cha Rwanda ‘Amavubi’.

Kutokana na mazoezi ya Aussems yanayoendelea, ukizingatia kasi ya ufungaji ya Kagere na Okwi inafahamika, ni wazi kuwa timu zitakazokutana na Simba zijipange hasa, la sivyo, zinaweza kujikuta ‘zikioga’ mabao’.

Na kwa kuwa mwishoni mwa mwezi huu, yaani Septemba 30, kutakuwa na pambano la kukata na shoka la watani wa jadi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, basi Yanga watalazimika kujipanga kisawasawa kuepuka aibu ya mabao itakayowachanganya na hata kusahau makwao.

Japo Aussems amekuwa akizuga kutoifikiria Yanga, lakini ukweli ni kwamba Wekundu wa Msimbazi hao wamejipanga hasa kupeleka ‘msiba’ Jangwani.

Mmoja wa viongozi wa Wekundu wa Msimbazi hao ambaye hakutaka jina lake kuwekwa hadharani, aliliambia BINGWA akisema: “Tunaisubiri kwa hamu sana Septemba 30, tunaamini siku hiyo itakuwa ya kukumbukwa na watu wa Yanga kizazi hadi kizazi kutokana na kile tutakachowafanyia.”

Mara ya mwisho Simba na Yanga zilipokutana ilikuwa ni Aprili 29, mwaka huu ambapo Wekundu wa Msimbazi walishinda bao 1-0, shujaa wao akiwa ni Erasto Nyoni.

Pamoja na yote hayo, Yanga bado inahaha kulipiza kisasi cha kufungwa mabao 6-0 na watani wao hao wa jadi mwaka 1977.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -