Wednesday, October 28, 2020

TUNALITUMBUKIZA SOKA LETU SHIMONI TUKIWA TUNAONA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA EZEKIEL TENDWA


AGOSTI 29 mwaka huu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini, Wilfred Kidau, alijitokeza mbele ya Watanzania akitangaza maamuzi ya Emmanuel Amunike, kuwapiga pini wachezaji sita wa Simba kati ya saba, kwenye kikosi cha Stars.

Wachezaji hao wa Simba, walipigwa ‘stop’ kutokana na kuchelewa kuripoti kambini kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na kocha, Amunike, ambaye ndiye mwenye jukumu kubwa la kuhakikisha timu yetu inapiga hatua mbele.

Wachezaji hao ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco pamoja na Shiza Kichuya huku mwenzao, Aishi Manula, ambaye ni kipa namba moja Stars na Simba, akiepuka adhabu hiyo baada ya yeye kuwahi kama ilivyotakiwa.

Baada ya kocha kusimamia msimamo wake huo, yaliibuka makundi mawili, moja likimuunga mkono na lingine likionekana kukerwa na kitendo hicho.

Nilipitia kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii nikagundua kuwa idadi kubwa ya mashabiki hasa waliojitambulisha kama wa Simba wakisema hawataiunga mkono Stars kwa sababu wachezaji wao wameenguliwa.

Yaani baadhi ya mashabiki hao wamediriki kusema, wanataka Stars ipate matokeo mabaya katika mchezo wao wa leo dhidi ya Uganda ‘The Cranes’.

Mchezo huo muhimu wa kutafuta tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani nchini Cameroon, utachezwa Uwanja wa Mandela, Namboole.

Wakati baadhi ya mashabiki hao wakidai kuwa wanataka Stars wapate matokeo mabaya, walijitokeza wengine wakidai kuwa hata timu hiyo ifungwe mabao mengi poa tu ilimradi kocha amewatimua wachezaji hao wa Simba.

Baadhi ya mashabiki hao, ambao nao wengi wanaonekana ni wale wa upande wa pili wakidai kuwa Stars kufungwa na Uganda si jambo la kushangaza na haitakuwa ajabu, isipokuwa wao kilichowafurahisha ni baada ya Amunike kuchukua hatua kali.

Baada ya mabishano hayo, haukupita muda mrefu tukamsikia Amunike akitumia uungwana kuwasamehe wachezaji hao wa Simba, lakini hakuwajumuisha katika mchezo wa leo kwani alikwisha kuwachagua wengine kuziba nafasi zao.

Kocha huyo ambaye ni moja ya wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na Barcelona ya nchini Hispania, waliocheza kwa kiwango kikubwa, aliwaambia wachezaji hao wa Simba kwamba atawaita tena kama wataonyesha uwezo mkubwa kwenye timu yao.

Baada ya kauli hiyo ya msamaha kwa Amunike, nikajua mambo yamekwisha na hata wale mashabiki waliokuwa wameleta mgawanyiko watakuwa wamerudi na sasa tutakuwa kitu kimoja.

Hata hivyo, jana nilishangaa kuona baadhi ya mashabiki wakibishania tena jambo hilo hilo, wengine wakidai kuwa wanataka Stars ipokee kichapo kutoka kwa Uganda, huku wengine wakisema potelea mbali ilimradi yaliyotokea yametokea.

Nilikuwa pale Kibamba njia panda ya Shule kwenye kituo cha daladala, nikisubiri gari ili kuwahi ofisini kwangu kuendelea na majukumu kama ilivyo kawaida ndipo nikakuta mjadala huo wakati mashabiki hao wakipitia magazeti mbalimbali kwenye meza yanapouzwa.

Wapo mashabiki wa Simba ambao wengi walisema lazima Stars ifungwe, wakionyesha bado wanakerwa kutokana na wachezaji wao wengi kuenguliwa huku wale wa Yanga wakidai kuwa hata wakifungwa si jambo geni.

Hao ninaosema ni mashabiki wa Simba ni kwa sababu nawajua na hao ninaowasema ni Yanga ni kwa sababu pia nawajua, ndiyo maana nayasema haya kwa uhakika bila kupepesa macho.

Hapa lazima niseme wazi kwamba, mashabiki wa hizi klabu kongwe, wanaleta mgawanyiko usiokuwa na tija kabisa kwenye soka letu na itakuwa vigumu sana kupiga hatua mbele. Tutaendelea kubaki nyuma mpaka tukome.

Jambo la kushangaza hapa ni kwamba, wale wa Simba wanadhani lazima Stars ipoteze mbele ya Uganda na wale wa Yanga wanasema hata ikifungwa mabao 8-0, halitakuwa jambo la kushangaza.

Kwa namna nilivyofuatilia mijadala hii, idadi kubwa wanafikiri lazima Stars ifungwe lakini kila mmoja akiwa na mawazo yake. Wale wa Simba hawana sababu nyingine isipokuwa ni wachezaji wao kuenguliwa na wale wa Yanga wakidai miaka yote Stars wanafungwa, wakiwamo wachezaji hao sasa itashangaza vipi tukipokea kipigo.

Nilichokuwa nawaza mimi ni kwamba hii ni timu ya Taifa ambayo mchezaji yeyote anaweza akaichezea. Yaani mchezaji wa Biashara, Tukuyu Stars, Mlandege hata wa Kibamba United, anaweza akaitwa na wote tukaunga mkono.

Tatizo la mashabiki wa Tanzania wanataka Yanga wakiitwa wachezaji saba, Simba nao waitwe saba na wote wapate nafasi ya kucheza kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Stars si lazima waitwe wachezaji kutoka Simba na Yanga. Hata timu nyingine wanaweza wakaitwa na mambo yakaenda sawa. Kutaka makocha wafanye kama mashabiki wanavyotaka ni kulikosea adabu soka letu, ni kurudisha nyuma maendeleo ya mpira wetu.

Ligi Kuu ya Tanzania, inazo jumla ya timu 20 ambazo zina zaidi ya wachezaji 500. Hapa nimeondoa wale wachache wa kigeni, sasa wachezaji zaidi ya 500 hiyo inamaanisha kuwa tuna hazina kubwa na isiwe nongwa kama shabiki ataona mchezaji anayempenda hajaitwa.

Nakumbuka kuna kipindi cha Marcio Maximo, kulikuwa na umoja wa hali ya juu na tukaona namna tulivyokuwa tukipiga hatua mbele kidogo kidogo, lakini ghafla tukarudi tulikotoka na tutarudi zaidi kama hali yenyewe itakuwa hii. Tuwe wazalendo jamani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -