Sunday, October 25, 2020

MSUVA AFANYIWA KITU ‘BAB KUBWA’ KAMPALA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MWAMVITA MTANDA


 

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza, amemfanyia jambo la kiungwana mno aliyekuwa winga wa timu hiyo, Simon Msuva, wawili hao walipokutana jijini Kampala, wiki iliyopita.

Msuva alikuwa jijini humo akiwa na kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars iliyokwenda huko kuvaana na Uganda ‘The Cranes’ katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita, timu hizo zilitoka suluhu.

Ikumbukwe kuwa Kiiza na Msuva waliwahi kucheza pamoja Yanga, hivyo kukutana kwao, kulikumbushia enzi zao walipokuwa wakikipiga Jangwani.

Kwa sasa Msuva anachezea kikosi cha Difaa El Jadidi ya Morocco, huku Kiiza akiwa hana timu baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya kikosi cha El Hilal El Obeid ya Sudan.

Tangu alipoingia Uganda, Kiiza alikuwa karibu mno na Msuva, ikiwa hivyo hadi baada ya mechi kati ya Stars na The Cranes.

Akizungumza na BINGWA kabla ya kuelekea Morocco, Msuva alisema baada ya kikosi cha Stars kurejea nchini, angejikuta akiwa mpweke, lakini anashukuru kwa kitendo cha Kiiza kumwonyesha upendo wa hali ya juu.

Alisema kuwa mshambuliaji huyo aliyewahi pia kukipiga Simba, alimfuata hotelini walikofikia Stars na kumpeleka katika maeneo ya vivutio ya nchini Uganda na kupata faraja mno.

“Sikuwa na furaha nilipoona wenzangu wanaondoka na nilikuwa bado nasubiri ndege ya Jumatatu, nashukuru Kiiza  alinipigia simu na kuniambia atakuja kunichukua akanitembeze.

“Ni mtu wa pekee kwa sababu ameacha mambo yake na kunithamini mimi, si jambo la kawaida,” alisema Msuva.

Wakati huo huo, Msuva alisema ana kibarua kizito cha kukabiliana na michuano ya Ligi Kuu nchini Morocco iliyoanza kutimua vumbi wiki iliyopita pamoja na mechi nyingine za kimataifa.

“Kilichokuwa kinaniumiza kichwa zaidi ni hii mechi ya Uganda, ilikuwa ngumu sana lakini tunashukuru kwa tulichokipata, sina muda tena wa kupumzika, nahitaji kupambana kuisaidia timu yangu,” alisema Msuva.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -