Tuesday, October 20, 2020

YANGA IMENOGA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

WINFRIDA MTOI


 

Yanga imewapa furaha mashabiki na wanachama wao baada ya jana kuvuna ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Ushindi huo umeiwezesha Yanga kuchupa kutoka nafasi ya 12 hadi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo, baada ya kufikisha pointi sita kutokana na michezo miwili.

Hata hivyo, furaha ya watu wa Yanga imeonekana kuingia doa kutokana na kitendo cha timu yao kuruhusu kufungwa mabao matatu, tena na mchezaji mmoja, Alex Kitenge, aliyepiga ‘hat-trick’ na kuondoka uwanjani na mpira.

Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi, alikuwa ni Mrisho Ngassa aliyeipatia Yanga bao la kwanza dakika ya kwanza baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Ibrahim Ajib.

Bao hilo lilidumu hadi dakika ya 15 pale Kitenge alipoisawazishia Stand United, akiitumia vema pasi kutoka kwa Jacob Massawe, kuukwamisha mpira nyavuni, kumwacha kipa wa Yanga, Kindoki Nkizi akiwa amesimama anashangaa.

Dakika mbili baadaye, Kitenge nusura afunge bao la pili pale alipopiga shuti kali lililotoka nje.

Yanga walijibu shambulizi hilo dakika 19 pale kiungo wao, Pappy Tshishimbi alipokosa bao la wazi kwa shuti lake kutoka nje kidogo ya goli baada ya kupokea pasi kutoka kwa Deus Kaseke.

Washambuliaji wa Yanga ambao jana walionekana kuwa na uchu wa mabao, waliendeleza mashambulizi langoni mwa Stand United na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 32, mfungaji akiwa ni Ajib aliyemtungua kipa wa wapinzani wao hao, akiwa nje kidogo ya 18 baada ya kuinasa pasi ya ya Tshishimbi.

Yanga walizidisha mashambulizi lango mwa wapinzani wao hao na hatimaye kupata bao la tatu katika dakika ya 34, lililowekwa kimiani kwa kisigino na beki wa kati, Andrew Vincent ‘Dante’.

Bao hilo la kiufundi lilitokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ajib ambao kabla ya kumfikia mfungaji, ulimbabatiza kipa wa Stand United, Mohammed Makaka.

Dakika ya 45, mwamuzi wa mchezo huo, Benedict Magai kutoka Mbeya, alimwonyesha kadi ya njano beki wa Yanga, Paulo Godfrey baada ya kumfanyia madhambi Sixtus Sabilo.

Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, Yanga wakitaka kuongeza mabao zaidi, huku Stand United wakihaha kusawazisha.

Dakika ya 46, Tshishimbi alikosa bao kwa kupiga shuti pembeni, kabla ya Sabilo kuikosesha Stand bao kwa kupiga shuti lilikwenda pembeni ya lango dakika mbili bvaadaye.

Katika dakika ya 49, Kitenge alikaribia kuifungia timu yake bao, lakini shuti lake lililotokana na pasi ya Sabilo, lilipaa.

Kocha wa Stand United, Armas Niyongabo, alifanya mabadiliko dakika ya 54 kwa kumtoa Datius Peter na kumwingiza Charles Chinonso.

Dakika tatu baada ya mabadiliko hayo, Kaseke aliifungia Yanga bao la nne kutokana na pasi ya Ngassa.

Bao hilo lilionekana kuwafanya Yanga kubweteka hali iliyowapa nguvu Stand United kushambuliaji kwa nguvu na kuvuna mabao mawili zaidi kupitia kwa Kitenge, likiwamo la pili lililotokana na mpira uliotemwa na Nkizi.

Kwa ujumla, Yanga jana walitengeneza nafasi ntyingi za mabao, lakini washambuliaji wao, akiwamo Herieter Makambo, walishindwa kuzitumia.

Lakini pia, mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kipindi cha pili, yalionekana kuigharimu mno Yanga kwani ndiyo yaliyowawezesha Stand United kuvuna mabao mawili.

Katika mabadiliko hayo, Zahera aliwatoa Ajib na Ngassa na kuwaingiza Yusuf Mhilu na Rafael Daudi.

Akizungumzia mchezo huo, Zahera alisema kuwa kipa wao, Nkizi alikosa umakini, huku Kitenge akionekana kufurahishwa na ‘hat-trick’ yake, akitamba kuwa si mara ya kwanza kufanya hivyo kwani amekuwa akicheka mno na nyavu katika kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi.

YANGA: Klaus Kindoki, Paulo Nyanganya, Gadiel Michael, Andrew Vincent,  Kelvin Yondan, Feisal Salum, Mrisho Ngassa/Rafael Daudi, Papy Tshishimbi,  Heritier Makambo, Ibrahim Ajib/Yusuph Mhilu na Deus Kaseke.

STAND UNITED: Mohammed Makaka, Bigirimana Ramadhan,  Niyonkuru Nassor, Ndoriyobija Eric, Erick Mulilo, Erick Mbirizi, Datius Peter, Jacob Massawe, Alex Kitenge, Hafidh Mussa na Sixtus Sabilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -