Tuesday, October 20, 2020

HOFU, MATA AWAGWAYA WAPINZANI WA MAN UTD LIGI YA MABINGWA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

MANCHESTER, England


 

BAADA ya kushuhudia mwanzo mgumu katika Ligi Kuu England msimu huu, kikosi cha Man United kinatarajia kuyageukia na mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakianza kuitupa karata yao ya kwanza kesho.

Man Utd itaanza hatua ya makundi ugenini dhidi ya timu ya Young Boys ya Uswisi, ikiwa ni moja kati ya mitanange sita watakayoshuka dimbani katika Kundi H lenye timu za Juventus na Valencia.

Kuelekea mchezo huo, kiungo wa Man Utd, Juan Mata, amewaonya nyota wenzake wa kikosi hicho na kuwaambia wazi kwamba kama kuna kosa kubwa watakalolifanya kesho ni kuidharau Young Boys.

Licha ya kuwa timu hiyo ya Young Boys haionekani kama itatoa upinzani katika kundi lao hilo, Mata anaamini wataingia uwanjani kesho kwa ajili ya kuionyesha United kwamba na wao wanaweza.

“Ligi ya Mabingwa imerudi na tupo tayari kuhakikisha tunafanya vizuri. Kikubwa ni kuwaheshimu wapinzani, tutafanya kosa kubwa sana kuwadharau Young Boys eti kwa sababu hawana jina kubwa Ulaya,” alisema Mata.

“Heshima yetu haitaenda kwa Young Boys pekee, pia na vigogo wengine tuliopangwa nao katika kundi letu. Nauona mwanzo mgumu kwa upande wetu,” aliongeza Mhispania huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -