Saturday, October 31, 2020

YANGA YAKATA NGEBE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI


TIMU ya Yanga imeendeleza makali katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu na kwa mara ya kwanza tangu mwishoni mwa msimu 2016/17 imekamata usukani wa ligi hiyo baada ya kuifunga Coastal Union bao 1-0.

Ushindi huo unawafanya Yanga kukata ngebe za mahasimu wao wa jadi Simba ambao leo wanaikabili Mbao FC katika mchezo utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Yanga imefikisha pointi tisa sawa na JKT Tanzania lakini wakitofautiana kwa wastani wa mabao ya kufungwa na kufunga.

Katika mchezo wa jana uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, bao la pekee lililowapa Yanga pointi tatu na kupanda kileleni mwa msimamo lilifungwa na mshambuliaji wao raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Heriter Makambo.

Bao hilo lililopatikana dakika ya 11 ni kazi nzuri ya kiungo Ibrahim Ajib aliyemtengenezea pande nzuri Makambo na kufunga kwa ustadi akitumia mguu wake wa kushoto.

Awali katika dakika ya sita, Yanga walifanya shambulizi kupitia Makambo ambaye alipokea krosi ya Gardiel Michael lakini mpira alioupiga kwa kichwa ulitoka nje ya lango.

Dakika ya 21, Ajib nusura aifungie Yanga bao la pili kwa shuti baada ya kupokea pasi Papy Tshishimbi lakini mpira ulitoka nje.

Coastal Union nao walikuja juu ambapo dakika ya 26 Andrew Simchimba aliunasa mpira uliokuwa unarudishwa langoni na mabeki Yanga na kupiga shuti ambalo lilidakwa na kipa Klaus Kindoki na dakika 37 alifanya shambulizi la kushtukiza lakini mpira ukatoka nje.

Dakika chache kabla ya mapumziko, Coastal Union walicharuka kusaka bao la kusawazisha lakini mipango yao ilivuruguka kutokana na safu ya ulinzi ya Yanga kusimama imara.

Kipindi cha pili kilianza kwa Coastal Union kufanya mabadiliko ya kumtoa Athuman Idd ‘Chuji’ na kuingia Mtenje Juma, huku Yanga wakimtoa Mrisho Ngassa dakika ya 58 na nafasi yake kuchukuliwa na Matheo Antony.

Dakika ya 51, mlinzi wa Yanga, Kelvin Yondani, alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Ayub Lyanga na dakika 53 AdeyunAhmed alionywa kwa kadi ya njano kutokana rafu aliyomchezea Deus Kaseke.

Coastal Union walikosa bao la wa wazi dakika ya 61 baada ya Simchimba aliyekuwa mwiba kwa mabeki wa Yanga kushindwa kuunganisha vyema kwa kichwa krosi iliyopigwa na Adeyun.

Wakati mashabulizi yakiendelea, Yanga walimtoa Makambo dakika ya 65 baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Amiss Tambwe na dakika ya 75 alitoka Kaseke na kuingia Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

Katika mechi nyingine za Ligi Kuu Bara zilizochezwa jana, Azam FC ililazimisha sare ya bila kufungana na Biashara United huku JKT Tanzania nayo ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mwadui.

Mbeya City iliifunga Ruvu Shooting mabao 4-2 wakati Ndanda FC ikiibamiza Mtibwa Sugar mabao 2-1 na Lipuli FC iliichapa Alliance FC bao 1-0.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -