Friday, October 23, 2020

KWANINI NYOTA SINGIDA UNITED WANAKACHA?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SALMA MPELI


UPO msemo wa Kiswahili unaosema ‘mficha maradhi kifo humuumbua’, kauli hii huenda ikajidhihirisha kwa Singida United ambao msimu huu wanapitia changamoto nyingi.

Singida United ikiwa inashiriki kwa mara ya pili Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kurejea msimu uliopita, kwa sasa imecheza michezo minne ikishinda miwili, sare moja na kufungwa mmoja .

Hata hivyo, matarajio ya mashabiki wengi kuona timu hiyo ikiendelea kuwa tishio yameanza kufifia kutokana na uendeshaji wake.

Kwa sasa Singida ina matatizo mengi ambayo yamesababisha wachezaji wengi mahiri kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Mishahara ya wachezaji na fedha zao za usajili inatajwa kuwa sababu zinazowafanya nyota wengi kuikacha timu hiyo.

Pamoja na uongozi wa timu hiyo kupitia Mkurugenzi wake ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Festo Sanga, hawataki kusema ukweli kuhusu madai ya baadhi ya wachezaji, lakini kinachozungumzwa na baadhi ya wachezaji kinaweza kuwa ndio ukweli wenyewe.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kwamba aliyekuwa kipa wa timu hiyo, Manyika Peter, kajiengua kuitumikia Singida kutokana na kile kinachodaiwa ni kushindwa kulipwa fedha zake.

Lakini Manyika si mchezaji wa kwanza kuachana na timu hiyo tangu ilipomalizika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, kwani amefuata nyayo za wachezaji wenzake takribani watano ambao waliachana na timu hiyo kwa sababu ya mishahara na fedha za usajili.

Licha ya kwamba uongozi wa Singida  United hautaki kuzungumzia tatizo la ndani ya timu hiyo, lakini taarifa zilizopo ni kwamba wachezaji kama Danny Ussengimana, Michael Rusheshangoga, Papy Kambale, Kigi Makasi na Said Lubawa, wote waliamua kuachana na timu hiyo kwa madai hayo.

Lakini zipo taarifa kwamba, beki wa timu hiyo, Miraji Adam, hajaungana na kikosi hicho tangu ilipoanza Ligi Kuu Bara msimu huu kwa sababu zile zile za madai ya mishahara na fedha za usajili.

Inasemekana alikuwa kwao mkoani Morogoro akiendelea na mambo yake mengine hadi pale uongozi utakapomlipa stahiki zake ili aweze kurudi kikosini.

Wakati Singida United wakiendelea kuweka usiri katika jambo hilo, imebainika kwamba beki wa kimataifa wa timu hiyo, Mganda, Shafik Batambuze, amegoma kurudi kuitumikia  klabu hiyo.

Zipo habari kwamba Batambuze hajaungana na timu hiyo tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu na kubwa likitajwa ni madai ya fedha zake za usajili.

Ni fedheha kubwa kwa Singida United kukimbiwa na wachezaji wakati jezi ya timu hiyo imezaa nembo kibao za wadhamini ukilinganisha na timu nyingine.

Walikuwa na mwanzo mzuri na pengine katika vichwa vya wadau wengi wa soka nchini walianza kuifikiria Singida United imerejea kuonyesha ushindani wa kweli wa soka.

Tatizo linalotajwa na wachezaji kushindwa kulipwa mishahara na fedha zao za usajili linazidi kuwa kubwa.

Wachezaji wengi wamekuwa wakilalamikia juu ya viongozi kujitangaza wana maisha mazuri ndani ya Singida United huku kukiwa hakuna ukweli wowote.

Nadhani si dhambi kusema ukweli kuwa wachezaji wanadai kuliko viongozi kuendelea kusema Singida United iko vizuri wakati wachezaji wanapata maumivu.

Lakini najiuliza kwanini wachezaji nyota wa Singida United wanaikacha timu hiyo?

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -