Wednesday, October 21, 2020

HUKU KWENYE LIGI YA EUROPA KUNA WENYEWE

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England


NI msimu mpya wa Ligi ya Europa (Uefa ndogo) 2018/19 hatua ya makundi, ikitarajiwa kuanza leo usiku kwa vigogo mbalimbali barani Ulaya kutunishiana misuli kwa lengo la kuwania ubingwa wa michuano hiyo.

Ieleweke kuwa licha ya kwamba Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo ni mashindano makubwa kwa ngazi ya klabu barani humo, yalianza kwa kasi lakini Ligi ya Europa nayo haitakosa utamu wake.

Baadhi ya timu kali zilizomo humo ni Arsenal, Chelsea, AC Milan na Sevilla, hao wakiwa ni vigogo wachache kati ya wale ambao watapambana kuanzia leo hadi ifikapo Mei mwakani.

Kuelekea mechi za leo, haya hapa mambo muhimu ya kuyatupia macho:

Kwa Emery, Europa ni nyumbani

Arsenal vVorskla

(Emirates Stadium)

Kocha huyo wa Arsenal, Unai Emery, ana rekodi nzuri ya kunyakua taji la michuano hiyo mara tatu mfululizo akiwa na kikosi cha Sevilla.

Na ikumbukwe pia ametua kwenye timu hiyo yenye makazi yake katika viunga vya Emirates, ambayo msimu uliopita wa Europa waliishia katika hatua ya nusu fainali, hivyo wana nafasi ya kuboresha walipoishia.

Kwa uzoefu wa Emery na jinsi anavyojaribu kuitengeneza Arsenal kuwa timu tishio, iwapo wataweza kuvuka hatua ya makundi na hatimaye mtoano hadi fainali, Arsenal itapata faida kubwa mno.

Ikumbukwe kuwa kiasi cha fedha ambacho timu inapata katika Ligi ya Europa hakilingani uzito wa fedha ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na mashindano mengine ya bara hilo.

Kama Arsenal watatinga fainali ya michuano hiyo na kutwaa taji, watakabidhiwa kitita cha euro milioni 25 (Sh bilioni 66), tofauti na upande wa pili ambao bingwa wake hupewa mara tano ya kiasi hicho cha fedha.

Ni muhimu zaidi kwa Arseanal kunyakua ubingwa wa Europa msimu huu, kwani ndio tiketi yao ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya ambako ndiko kwenye heshima zaidi na pia itawanenepesha kiuchumi.

 Chelsea dhidi ya ‘masela’ PAOK

PAOK v Chelsea

(Toumba Stadium)

Ligi ya Europa ni michuano yenye msisimko wa kipekee kuanzia timu shiriki pamoja na mashabiki wake wanaojaza viwanja vya soka na kuvipamba kwa aina mbalimbali za ushangiliaji.

Msimu huu Chelsea watashiriki ligi hiyo na wataanza kufungua pazia dhidi ya ‘masela’ wa Ugiriki, PAOK, timu ambayo ilikumbwa na sekeseke zito miezi kadhaa iliyopita.

Mabingwa wa michuano hiyo ya Europa mwaka 2013, Chelsea, wategemee mapokezi ya ‘kutisha’ watakapoingia kwenye uwanja wa ugenini wa PAOK, kufungua pazia la Kundi L.

Wengi mtakumbuka tukio lililoripotiwa miezi sita iliyopita la Rais wa PAOK, Ivan Savvidis, kuvamia uwanja na bastola kiunoni mwake wakati timu yake hiyo ilipokuwa ikichuana na AEK Athens.

Kitendo hicho kilisababisha Ligi Kuu Ugiriki kusimamishwa kwa muda, huku rais huyo naye akikumbana na adhabu PAOK ikimaliza ligi katika nafasi ya pili lakini ilishindwa kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa, baada ya kupoteza kwa Benfica kwenye mchezo wa kufuzu.

Si tukio hilo tu la Rais Savvidis kuvamia uwanja ambalo linaweza kuitisha timu ngeni, bali pia uwanja wa nyumbani wa PAO, Toumba, wenye uwezo wa kuingiza watu 29,000.

Uwanja huo unatambulika kwa mazingira yake ya kuvutia mno, huku mashabiki wake wakiwa na aina ya kipekee ya ushangiliaji.

Mwanzo mgumu kwa Gerrard

Villarreal v Rangers

(Estadio de la Ceramica)

Gwiji la soka kutoka England, Steven Gerrard, naye hatabaki nyuma katika mashindano hayo ya Europa akiwa na kikosi cha Rangers ya Scotland.

Ni mafanikio makubwa kwa Rangers kutinga hatua ya makundi Ligi ya Europa huku Gerrard akiwa ndio kwanza amekabidhiwa jukumu la kuiongoza msimu huu.

Klabu hiyo yenye makazi yake jijini Glasgow, ilitinga hatua hiyo kupitia mechi za kufuzu kwa mara ya kwanza tangu waliposhiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2010-11.

Vita ya Daudi, Goliati

F91 Dudelange v AC Milan

(Stade Jos Nosbaum)

Ndio, ni AC Milan dhidi ya Dudelange. Umewahi kuisikia hiyo timu ya pili? Subiri uambiwe.

Msimu huu utakuwa ni wa kwanza katika historia ya klabu ya Dudelange kutoka Luxembourg kucheza hatua ya makundi katika Ligi ya Europa tena dhidi ya vigogo AC Milan.

Hakika ni mechi ambayo ingeweka historia kubwa hata kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ndio maana mpambano baina yao na Milan umefananishwa na wa Daudi na Goliati.

Timu hiyo iliweza kuingia Europa baada ya kushindwa katika mechi za kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na bado ni mafanikio makubwa kwao.

Marseille kucheza bila mashabiki

Marseille v Frankfurt

(Velodrome)

Wababe wa Ufaransa, Marseille, wanakumbukwa kwa kiwango bora walichokionesha msimu uliopita hadi walipoweza kutinga fainali ambayo hata hivyo walipoteza dhidi ya Atletico Madrid.

Lakini kwa bahati mbaya msimu wao mpya utaanza bila kuwa na mashabiki katika uwanja wao wa nyumbani, kutokana na tabia za mashabiki hao walizoonesha katika fainali hiyo.

Licha ya rekodi yao kuwa nzuri wawapo katika dimba lao la nyumbani, Marseille huenda wakajikuta wakipata shida dhidi ya mabingwa hao wa Kombe la Ujerumani msimu uliopita kutokana na kuikosa sapoti ya mashabiki wao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -