Monday, October 26, 2020

PAPAA ZAHERA AWASHUKIA WACHEZAJI

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA MWAMVITA MTANDA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ‘Papaa’, amewashukia wachezaji wa timu hiyo na kusema kuwa hawana nidhamu ya mpira wanapokuwa uwanjani.

Zahera alisema hayo juzi, baada ya mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, ambayo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mtanange huo, kikosi cha Yanga kilijitahidi kupambana kwa lengo la kutaka kufunga mabao mengi nyumbani, lakini mara kadhaa wachezaji walionekana wakipoteza mipira.

Akizungumza na BINGWA juzi, kocha huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alisema kuwa, sababu kubwa inayowafanya wachezaji wake wasicheze mchezo wa kuridhisha ni kutokuwa na nidhamu ya mpira.

“Unajua bado sijaona ile kasi ambayo nahitaji uwanjani, wengi hawana utulivu, maana unakuta mchezaji hatulii kuangalia mwelekeo wa mpira, badala yake anakuwa anahangaika huku na kule, kwa staili hii hawawezi kufanya vizuri kama hawatakubali kubadilika,” alisema Zahera.

Aidha, Zahera aliwataja baadhi ya wachezaji ambao kwa sasa wamepoteza morali ya mchezo na kutokuwa makini na miongoni mwao yupo kiungo mkabaji, Papy Tshishimbi, ambaye hata juzi alionekana kupoteza mpira mara mbili.

Zahera aliongeza kuwa, kiungo huyo anapaswa kubadilika, ili timu iweze kufanya vizuri kwa sababu naye ni miongoni mwa wachezaji ambao ni tegemeo.

“Tshishimbi ni mchezaji mzuri, lakini amekuwa hana utulivu, anakimbia kila mahali na hajui wapi mpira unatakiwa kwenda, pia anatumia nguvu nyingi badala ya akili.

“Kama akibadilika atafanya vizuri katika mechi zijazo, kwani bado Ligi Kuu ni ngumu na kila timu timu tunayokutana nayo inahitaji ushindi, hivyo ni lazima tupambane,” alisema.

Kwa upande wake Tshishimbi, alisema si kila mechi mchezaji anaweza kufanya vizuri, ila upepo unaweza kubadilika kutokana na viwango vya wachezaji wa timu pinzani.

“Natambua kilichoniweka hapa ni kuisaidia timu, lakini si kila siku naweza kufanya vizuri, lakini ninachojua ni kwamba huwa najituma kwa namna niwezavyo ili kuhakikisha naisaidia timu yangu,” alisema Tshishimbi.

Hata hivyo, Tshishimbi alisema kutokana na kocha kuyaona mapungufu yake, kwa sasa anajipanga kuyarekebisha ili aweze kuwa imara zaidi kwa mechi zijazo.

“Huwa napenda kusikiliza sauti ya kocha, hasa kile anachoniambia, hivyo kwa kuwa amegundua makosa yangu ndiyo yamekuwa tatizo la mimi kutokucheza kwa kiwango nipo tayari kujirekebisha, nipo chini yake na nitatekeleza maelekezo ili niendelee kufanya vizuri,” alisema Tshishimbi.

Mchezo wa juzi ulikuwa wa tatu kwa Yanga tangu kuanza kwa Ligi Kuu msimu huu, ambapo katika mechi ya kwanza walishinda mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na baadaye kuichapa Stand United mabao 4-3.

Yanga sasa imejikusanyia pointi tisa kutokana na mechi tatu zilizochezwa, huku pia ikitarajiwa kushuka tena dimbani keshokutwa kumenyana na Singida United katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -