Thursday, October 29, 2020

NYIKA AKWAA KISIKI YANGA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

>>Ni baada ya kuomba huruma ya Bodi ya Wadhamini, aambiwa apambane na hali yake

NA HUSSEIN OMAR


MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika na wenzake ambao hadi sasa bado wapo madarakani ndani ya klabu hiyo baada ya wenzao kujiuzulu, wamekwaa kisiki katika harakati zao za kutaka kujinasua kwenye mkono wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Viongozi hao wanachunguzwa na Takukuru kubaini kama kuna rafu zozote wamecheza katika suala zima la fedha za klabu hiyo, kuanzia kwenye mchakato wa usajili wa wachezaji, mapato na matumizi ya fedha kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni hofu inayotokana na shutuma hizo, Nyika na wenzake walifunga safari kwenda Zanzibar kumwomba mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu hiyo, Mama Fatuma Karume, kukutana na wenzake kuona ni vipi wanaweza kuwasaidia kujinasua kutoka katika shutuma hizo.

Habari za ndani ya Yanga zililiambia BINGWA kuwa kwa takribani wiki mbili sasa viongozi hao walioitwa na kuhojiwa na Takukuru, wamekuwa wakihaha kufanya vikao kuona ni jinsi gani wanalimaliza tatizo hilo.

“Juzi kulikuwa kuna kikao pale Travertine Hoteli Magomeni ambapo Bodi ya Wadhamini na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji, walikutana kujadili uchaguzi lakini pia waliombwa kulitazama suala la Takukuru kwa jicho la tatu,” alisema mtoa habari wetu.

Alisema viongozi hao walifikia hatua hiyo wakihofia mambo yanaweza kuwa magumu kwao na kuomba Bodi ya Wadhamini ya Yanga, ikiongozwa na George Mkuchika, kuangalia kama inaweza kuwasaidia kimawazo na ushauri kuhusiana na suala lao hilo.

BINGWA lilimtafuta mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo, Jaji John Mkwawa, ambaye alitoa ushirikiano wa juu na kusema suala hilo wamelisikia kwa chini, lakini wao hawawezi kufanya lolote hivyo wamewaachia wenyewe Takukuru.

“Sisi hatuwezi kuingilia masuala ya Takukuru, wapo kisheria, lakini kwanini wawe na wasiwasi kama kweli si wahalifu, watulie tu uchunguzi upite kama kweli kulikuwepo na viashiria vya rushwa,” alisema Mkwawa.

Lakini kwa upande wake, mjumbe mwingine wa bodi hiyo, Francis Kifukwe, alisema suala hilo lipo lakini si sahihi kwa kipindi hiki kuliweka katika vyombo vya habari.

“Si vizuri kulizungumza sana katika vyombo vya habari, masuala haya yote yapo kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini, George Mkuchika,” alisema Kifukwe.

BINGWA lilipomtafuta Nyika kuzungumzia suala hilo, simu yake ilikuwa ikitumika kwa muda mrefu na hadi tunakwenda mitamboni, hakuweza kupatikana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -