Sunday, October 25, 2020

A-Z BIFU LA MBELGIJI, DJUMA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA WAANDISHI WETU


HATIMAYE ukweli wa sababu za Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, kutengwa ndani ya klabu hiyo umepatikana baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya waandishi wa BINGWA kwa wiki nzima.

Djuma amekuwa nje ya kikosi cha Simba kilichosafiri kwenda Mtwara kuvaana na Ndanda FC ya huko mwishoni mwa wiki iliyopita na hata safari ya Mwanza walikocheza na Mbao FC juzi Alhamisi.

Katika michezo yote hiyo miwili, Simba imeambulia pointi moja tu baada ya kupata suluhu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, mjini Mtwara na kupokea kipigo cha bao 1-0, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kitendo cha Simba kutopata matokeo mazuri katika mchezo wa Mtwara, kilipokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa timu hiyo, baadhi yao wakidai kuwa kukosekana kwa Djuma ndicho chanzo, wakati wengine wakiamini ni matokeo ya kimchezo tu.

Wanaosingizia kukosekana kwa Djuma wanadai kuwa kocha huyo ndiye aliyewazoea zaidi wachezaji hali inayomwezesha kujua jinsi ya kuwatumia ili kupata matokeo mazuri, lakini pia wakisema kuwa ‘amshaamsha’ ya Mrundi huyo husaidia kuwapandisha mzuka wachezaji kusaka mabao pale wanapokuwa nyuma.

Mashabiki hao wanadai kuwa kitendo cha Djuma kukosekana katika kikosi chao, ni pengo kubwa kwa wachezaji wao na timu kwa ujumla kwani kocha huyo anaifahamu vizuri zaidi timu kuliko bosi wake, Mbelgiji Patrick Aussems.

Juu ya kubakizwa kwa Djuma Dar es Salaam, ilielezwa kuwa hayo yalikuwa ni maelekezo ya bosi wake ili aendelee na programu za kuwanoa wachezaji wasiosafiri na timu pamoja na wale wa timu ya vijana.

Lakini kwa mujibu wa habari ‘zilizochimbwa’ hasa na timu ya waandishi wa BINGWA, kocha huyo msaidizi wa Simba, amewekwa pembeni makusudi kutokana na shutuma kede kede za kinidhamu zinazomkabili.

Katika mahojiano na watu mbalimbali ndani ya uongozi wa Simba lakini pia wachezaji wa timu hiyo, imebainika kuwa Djuma ameponzwa na kile kilichoelezwa kuwa ‘uswahili’ wake unaolenga kumfanya kuonekana yeye ni bora zaidi ya kocha mwingine yeyote yule anayetua Msimbazi.

Katika uchunguzi huo wa BINGWA uliohitimishwa juzi baada ya mchezo wa Simba na Mbao, mtoa habari wetu aliliambia gazeti hili kuwa pamoja na kufungwa, Aussems aliridhishwa na kiwango cha wachezaji wake.

“Mwalimu alisema timu ilicheza vizuri  lakini hatukuwa na bahati, tulifanya kosa moja likatugharimu, tukapoteza. Tulitengeneza nafasi tukashindwa kufunga, wenzetu wakatumia nafasi waliyoipata. Kwenye mchezo kuna mambo mengi, lakini pamoja na yote hayo, tumekubali matokeo. Tunajipanga kwa mchezo unaofuata,” kilisema chanzo chetu.

Juu ya shutuma dhidi ya Djuma, BINGWA limebaini kuwa kocha huyo anadaiwa kuharibu heshima ya klabu hiyo kwa kuwa na ‘urafiki’ uliopitiliza na watu mbalimbali.

“Tulivyokwenda Misri alikuwa akihangaika na simu muda wote. Masoud ana matatizo, wewe fikiria Omog (Joseph) amemlalamikia, Lechantre (Pierre) amelalamika na huyu amekuja juzi tu amelalamika, we mtu gani kila mtu anakulalamikia?” alisema mmoja wa vyanzo vyetu vya uhakika ndani ya Msimbazi.

Aliongeza: “Wakati mwingine timu inatakiwa kuondoka muda fulani, mfano saa nane kwenda mazoezini, utakuta yeye haonekani. Anaambiwa na mwalimu waondoke pamoja kwenda mazoezini, yeye anatangulia na akifika anafanya mazoezi peke yake.

“Lakini pia, kuna wakati mwalimu anamwambia fundisha hivi, yeye anafundisha anavyotaka. Kuna siku mwalimu anamwambia Kichuya (Shiza) acheze hivi, yeye anamwambia acheze tofauti na maelekezo ya mwalimu.

“Nyinyi hamumjui, Masoud ana matatizo sana. Tulipokuwa Djibouti, alikuwa anasimama simama kila wakati, timu ikawa inacheza vizuri, mwalimu (Lechantre) alivyomzuia kusimama, timu ikacheza vibaya.

“Kuna siku mwalimu alitaka kumtoa Kichuya watu wakaonekana kutokubaliana naye, mwalimu akamuuliza (Kichuya) kwanini unacheza vile, akasema kocha Masoud kamwelekeza acheze vile. Hata wachezaji wengine wanamchukia kutokana na tabia yake hiyo.”

Habari zaidi zinadai kuwa Djuma amekuwa na tabia ya kupingana na Aussems katika mambo mengi, akipenda kuonekana yeye ni bora zaidi ya wengine.

“Kunapokuwa na kikao cha mechi, mwalimu anaweza kuweka plani zake halafu na yeye anafanya kikao kingine na wachezaji na kuwaelekeza vingine. Unakumbuka mechi ya Ngao ya Jamii (dhidi ya Mtibwa Sugar)? Kiongozi mmoja alimuuliza (Djuma), umeionaje timu, kocha akajibu si mumuulize mzungu wenu.”

Inaelezwa kuwa wakati mwingine Aussems anapofundisha wachezaji wake anazungumza kwa dakika mbili na wachezaji, halafu anapoambiwa atafsiri, yeye anaongea kwa dakika tano, hivyo watu kuhoji huwa anaongea nini cha ziada kama si kuwapotosha wachezaji!

Watu waliozungumza na BINGWA kwa nyakati tofauti kuelezea kinachoendelea kati ya Simba na Djuma, wamefunguka mengi ambayo hakuna anayeweza kuyavumilia ndani ya klabu hiyo.

“Wakati wa mechi, mwalimu huwa anamtaka Masoud kuisoma timu pinzani wakati yeye akiiangalia timu yetu, lakini baadaye akiulizwa (Djuma) amejifunza nini, anamjibu mwalimu ‘kwani na wewe si umeiona mechi’. Ana matatizo mengi sana Masoud, hatutaki tu kuyaweka wazi… hadi umefika wakati mwalimu amechoka.”

Mtu mwingine wa ndani ya Simba aliyehojiwa na BINGWA katikati ya wiki hii alihoji: “Kwanini hawa makocha wote walalamike. Tatizo yeye ana sumu, mwalimu akitaka wachezaji wacheze hivi, yeye anaelekeza vingine.

“Wakati wa chakula wachezaji wetu wanakula kwa pamoja na yeye anatakiwa kula pamoja na walimu wenzake, lakini anakuja na ‘headphone’ kama mchezaji. Halafu huwa anatukana wachezaji kuna mmoja alitukanwa hadi akalia hawapendi tabia zake, wanampenda mzungu, si unaona Mohammed Ibrahim ameanza kurudi, hata Salamba (Adam) anacheza, anawarudisha taratibu.

“(Mbelgiji) anamwambia Salamba muda wako bado, sasa hivi ajifunze kwa Okwi (Emmanuel) na Bocco (John), wachezaji anawachukulia kama watoto, anaongea nao kama mzazi, anawafundisha taratibu. Watu wanapigapiga kelele kwa kuwa hawajui matatizo ya Djuma.

“Mwalimu alimkataza kuongea na vyombo vya habari, lakini akawa anaendelea kuzungumza. Jiulize vyombo vya habari vilijuaje kama hatakwenda Mwanza kama si yeye aliyetoa siri?”

Wakati hayo yakitokea, Djuma ametokea kuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba kutokana na imani yao kuwa ndiye aliyechangia kuiwezesha timu yao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuusotea tangu msimu wa 2012/2013.

Pamoja na kubadilisha makocha kutoka nchi mbalimbali, lakini kwa kipindi chote hicho Simba haikufanikiwa kubeba ubingwa huo wa Bara hadi alivyotua Djuma ambaye baadaye aliletewa Kocha Mkuu, Mfaransa Lechantre.

Makocha waliopita Simba kabla ya Lechantre na Djuma ni Milovan Cirkovic (Serbia), Patrick Liewig (Ufaransa), Abdallah Kibadeni (Tanzania), Zdravko Logarusic (Croatia), Joseph Omog (Cameroon), Moses Basena na Jackson Mayanja, wote wa Uganda.

Baadhi ya mashabiki wa Simba wanaamini kuwa Djuma ndiye aliyefanikiwa kukata kiu yao kwa mfumo wake wa 3-5-2 ambao uliing’arisha timu yao na kubeba taji la Ligi Kuu Bara ambalo kwa mara ya mwisho walilibeba msimu wa 2011/12.

Djuma alikuja nchini kuchukua nafasi ya Mayanja na kuwa chini ya Omog, ambaye naye aliondoka na kumwacha mwenyewe kwenye timu.

Baadaye alitua Lechantre kuja kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, wakati huo Djuma ambaye ndiye alikuwa msaidizi alishaanza kuinoa timu hiyo na kushinda mechi takribani tatu.

BINGWA lilimtafuta Djuma kuzungumzia shutuma hizo dhidi yake lakini wakati wote amekuwa akisisitiza kuwa hawezi kuzungumza lolote kwani bosi wake, Aussems, ndiye mzungumzaji wa timu na anaheshimu hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -