Sunday, October 25, 2020

NDAYIRAGIJE ATAMBA KUIZIMA LIPULI FC

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SALMA MPELI

BAADA ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United, kocha wa timu ya KMC, Etienne Ndayiragije, amesema kuwa ushindi huo umewapa morali wachezaji wakati wakijiandaa kumenyana na Lipuli FC kesho.

Akizungumza na BINGWA, kocha huyo alisema ushindi walioupata umewapa mwanga na kuwafungulia njia, kwani tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu walikuwa wamecheza mechi nne na kupata sare tatu na kufungwa mmoja.

Aidha, alisema kuelekea mchezo wao dhidi ya Lipuli, anaamini wachezaji watacheza wakiwa na ari ile ile kama ilivyokuwa katika mechi ya Stand United ili waweze kupata ushindi kwa mara ya pili.

“Tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumanne (kesho) dhidi ya Lipuli, kikosi kipo katika hali nzuri na malengo yetu ni kuhakikisha hatupotezi mchezo wowote uliopo mbeleni ili kujiweka katika mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi,” alisema Ndayiragije.

Hata hivyo, Ndayiragije alikiri kuwa ligi ya msimu huu ni ngumu na kila timu imejipanga vizuri, hivyo licha ya kuumizwa na matokeo ya mechi zao za awali, wanatambua pia hiyo ni sehemu ya mchezo na watajipanga zaidi katika mwendelezo wa ligi hiyo.

KMC ambayo ni timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, baada ya ushindi wao wa kwanza dhidi ya Stand United sasa imefikisha pointi sita kutokana na mechi tano walizocheza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -