Friday, October 30, 2020

ZAHERA AISHTUKIA SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

HUSSEIN OMAR NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewashtukia wapinzani wao wa jadi, Simba ambao watakutana Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Baada ya miamba hiyo ya Tanzania kutoa dozi katika mechi nne

mfululizo, kocha huyo amegundua kuna mambo ambayo asipoyafanyia kazi anaweza kuwa kwenye wakati mgumu dhidi ya mahasimu wao.

Akizungumza na BINGWA jana, Zahera, amesema atakuwa na programu mbalimbali atakazofanya lakini kikubwa ni kuhakikisha wachezaji wanakuwa fiti kwa asilimia 100 kumudu upinzani dhidi ya Simba.

Zahera alisema katika mazoezi watakayofanya leo asubuhi ataanza na programu ya kuwaongezea pumzi wachezaji ambao wamekuwa wakishindwa kucheza dakika zote 90 bila kuchoka.

Hivyo kocha huyo amepanga mazoezi makali yatakayowafanya wawe fiti na kucheza mtanange huo bila ya kuchoka katika dakika zote akiamini hiyo ndiyo dawa ya kuendelea kutoa dozi Ligi Kuu na kuwachapa mahasimu wao.

“Mchezo dhidi ya Simba hautakuwa wa kawaida na natakiwa kufanya jambo. Kuna wachezaji ambao wamekuwa wakifika dakika 70 pumzi inakata, hao ndio naanza nao kwa siku hizi kadhaa,” alisema Zahera.

Pia Zahera, alisema mshambuliaji wake, Heritier Makambo na winga Mrisho Ngassa ambao waliukosa mchezo wa juzi dhidi ya Singida United walioshinda 2-0, watarejea kwenye kikosi hicho kuendelea na maandalizi wa mtanange huo.

Lakini Zahera alisema Thaban Kamusoko atabaki Dar es Salaam ili kuendelea na matibabu kwa kuwa jeraha lake si la kupona ndani ya wiki moja.

“Makambo na Ngassa, hali zao ziko vizuri na tutakuwa nao kambini, lakini mchezaji ambaye hatakuwapo ni Kamusoko kwa kuwa si mtu wakupona kwa sasa,” alisema Zahera.

Kikosi hicho cha Yanga kimeondoka jana kwenda Morogoro na leo asubuhi wataanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa watani wa jadi.

Akizungumza na BINGWA jana, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Thobias Lingarangara, alisema kwa sasa hakuna kulala, muda walionao hautoshi, hivyo ni lazima kwenda na kasi iliyopo kufanikisha malengo yao.

Alisema lengo kubwa walilojiwekea ni kushinda mechi hiyo ya Septemba 30, mwaka huu ili kuwaweka katika nafasi nzuri ya kushinda mechi zao 11 za nyumbani.

Lingarangara alisema licha ya kubanwa na ratiba, baada ya mchezo wa juzi na Singida United, walitaka timu iende moja kwa moja Pemba visiwani Zanzibar, lakini wameamua kwenda Morogoro.

“Tupo vizuri licha ya changamoto za hapa na pale, tuna uhakika wa kufanya vema dhidi ya Simba kwa kuwa tunaupa uzito mkubwa mchezo huo na ni muhimu kwetu,” alisema Lingarangara.

Alisema ni lazima wawafunge Simba ili kulinda heshima ya timu yao kwani tangu msimu wa mwaka 2016, hawajawahi kuonja ladha ya ushindi dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi.

Yanga wataweka kambi yao katika Hoteli ya Kings Way na watakuwa wanatumia Uwanja wa Jamhuri kufanyia mazoezi.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -