Tuesday, October 20, 2020

PROSPA OCHIMANA MKALI ANAYEKIMBIZA NA EKWUEME

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

Lagos, Nigeria

*Aliutunga wimbo huo baada ya CD kwenye gari kugoma

Prospa Ochimana (Tytman) wa Kogi nchini Nigeria, ni mmoja wa waimbaji wanaokuja kwa kasi kwenye muziki duniani.

Mwimbaji huyo ni mtunzi wa nyimbo, mwalimu na mwongozaji wa muziki.

Prospa amekuwa akihudhuria tamasha la muziki wa injili la Festival of Grace (FoG) ambalo limekuwa likihudhuriwa na waimbaji wakubwa kama Freke Umoh, Chris Morgan, Psalm Ebube, Elijah Oyelade na wengine wengi.

Katika wimbo wake wa ‘The Great IAM’, Prospa alielezea ukuu wa Mungu, akitumia kitabu cha Zaburi 104 ambayo inatilia mkazo ukuu na upendo wa Mungu. Kwenye wimbo huo, alienda mbali zaidi kuelezea nguvu na nafasi ya Mungu katika maisha yetu ya kila siku.

Alitukumbusha kwamba hatuna kitu kwenye maisha bila ya Mungu. Vyovyote tulivyo, chochote tulichonacho, bado Mungu anabakia mkuu.

‘The Great IAM’ ni wimbo ambao utajenga uhusiano wetu na Mungu kupitia njia ya kuabudu.

Kama una hasira, wimbo wa The Great Iam IAM ndio wa kusikiliza kwa kurudia na utakubadilisha.

Ukiachana na wimbo huo wa The Great Iam IAM, mwimbaji huyo anatamba na Ekwueme ambayo inafanya vizuri kila sehemu ikiwamo hapa nchini.

Akizungumzia kufanya vizuri kwa wimbo huo wa Ekwueme, Prospa anasema Yesu ndio amefanya wimbo huo utambe kila sehemu.

“Yesu ndio ameubariki Ekwueme. Nakumbuka kabisa wazo la wimbo hilo lilivyokuja, nilikuwa naendesha gari kwenda kanisani siku hiyo, nikajaribu kuweka muziki na redio yangu ya gari ikagoma. Hivyo, nikaamua kuimba na nilipofungua mdomo wangu Ekwueme ikaja,” anasema Prospa.

“Niliimba kwa muda, nikachukua simu na kujirekodi. Sikujua maana ya Ekwueme hivyo nikaulizia maana yake kutoka kwa marafiki zangu na Mungu akatusaidia wimbo huo ukasambaa ulimwenguni kote kama tunavyoona sasa.”

Anasema amefanya nyimbo nyingi za kabila lao la Igbo, lakini hakutegemea kuona kama anachokiona sasa, ingawa alijua ni wimbo mzuri.

Amesema amemshangaa sana Mungu kwa kile alichokifanya kwenye wimbo huo wa Ekwueme, akisema: “Ni maajabu makubwa kuona kile Mungu anaweza kufanya na mtu wake. Yesu anaufanya wimbo huo uzidi kupaa na jina lake kutukuzwa, sijafanya kitu chochote cha ajabu kuhusu wimbo huo, lakini Mungu mwenyewe ndio anafanya kila kitu. Ni wimbo wake, tunamwimbia yeye, anautangaza wimbo huo yeye mwenyewe. Yeye ndio promota mkubwa.”

Mashairi ya wimbo huo wa Ekwueme

Onye Nwe anyi Ezitewo (our God that sent)

Ndi Mmoziya ka ha nonyere anyi (His angels to come be with us)

You are The Living God oh..

Eze (King), No one like You

Ekwueme Ekwueme (The One who says and does it)

Ekwueme Ekwueme

You are the living God oh..

Eze (King), no one like You

Ekwueme Ekwueme (The One who says and does it)

Ekwueme Ekwueme

You are the living God oh..

Eze (King), no one like You

(Speaking in Tongues)

You are the living God oh..

Eze (King), no one like You

(Speaking in tongues)

Eze (King), no one like You

Verse 1

You’re my Healer, You are my Keeper

My Restorer, My Lifegiver

You are the living God oh..

Eze (King) no one like You

No one can do me like You do

No one can touch me like You do, God

You are the living God oh…

Eze (King) no one like You

You picked me from the miry clay, set my feet on the rock to stay

You’re my Promoter, You’re my Defender

You are the Living God oh…

Eze (King), No One like You

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -