Tuesday, October 27, 2020

ZAHERA ARUSHA DONGO SIMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI

KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewarushia dongo wenzake wa Simba kuwa hata siku moja hawawezi kukisoma kikosi chake.

Kauli hiyo ya Zahera imekuja kutokana na mpango wa makocha wa Simba wa kuisoma Yanga ilipokuwa ikivaana na Coastal Union na Singida United katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wakati kikosi cha Simba kikiwa safarini Mtwara kuvaana na Ndanda FC kabla ya kwenda Mwanza kukipiga na Mbao na baadaye Shinyanga kupambana na Mwadui, Kocha Msaidizi wa Wekundu wa Msimbazi hao, Masoud Djuma, alibaki Dar es Salaam ili kukisoma kikosi cha Yanga.

Haya yanadaiwa kuwa maelekezo ya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, aliyemtaka msaidizi wake huyo, Djuma, kubaki Dar es Salaam kuchunguza uchezaji na mbinu za Yanga kuelekea mchezo baina ya wakongwe hao wa soka nchini keshokutwa.

Akizungumzia mpango huo wa watani wao, Zahera ameliambia BINGWA kuwa hana hofu na Simba kwa sababu tayari anafahamu ni jinsi gani anaweza kuwasambaratisha Wekundu wa Msimbazi hao baada ya kuwasoma vilivyo kupitia mechi zao kadhaa.

Alisema hawezi kuwa na presha au kufuatilia mechi za wapinzani wao zaidi ya kuwajenga wachezaji wake tayari kuwafunga Simba Jumapili na hatimaye kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Zahera alibainisha kuwa hadi sasa amecheza mechi nne za Ligi Kuu Bara na ameshinda zote na hakuwahi kuomba mtu afuatilie michezo ya timu alizokutana nazo ili ampe ushauri wa kitu anachotakiwa kufanya.

“Sina ulazima wa kumwambia mtu afuatilie mechi halafu anipe ushauri kwa sababu tu ninacheza na Simba, hicho siwezi kufanya, Simba ni timu kama nyingine.

“Mbona nimecheza na Mtibwa Sugar, Stand United, Coastal Union na Singida United, nimepata matokeo niliyohitaji na sijaomba ushauri wa mtu yeyote zaidi ya kuwaandaa wachezaji wangu vile ninavyojua mimi?” alihoji Zahera.

Hata hivyo, alisema kuwa Simba wamejisumbua kupoteza muda wao kwenda uwanjani kukisoma kikosi chake ambacho alitamba hata siku moja hakiwezi kusomeka.

“Nina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa na shauku ya kufanya vizuri, hakuna anayeweza kuwasoma, leo tunacheza hivi, kesho vile…nani alitegemea Tambwe (Amissi) anaweza kufunga? Lakini ona jinsi alivyoifunga Singida United mabao mawili na kuipa timu yetu ushindi wa mabao 2-0 na pointi tatu.”

Juu ya maandalizi ya mchezo huo wa kukata na shoka, Zahera alisema anaendelea kuwanoa vilivyo wachezaji wake mjini Morogoro na kwamba kila mmoja anaonekana kuwa na shauku ya kufanya vizuri Jumapili.

“Morali ya wachezaji wote ipo juu, wanafanya mazoezi kwa bidii, naamini hawatawaangusha mashabiki wa Yanga Jumapili, waje uwanjani kwa wingi ili wawashangilie kwa nguvu wachezaji wao waweze kucheza kwa nguvu zao zote,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -