Friday, October 23, 2020

KAKOLONYA MTU NA NUSU

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ZAITUNI KIBWANA

UNAPOFANYA kitu na ukakubaklika na watu basi mtaani utaitwa ‘mtu na nu’ na hivyo ndivyo kipa wa Yanga, Beno Kakolanya alivyojipatia hilo jana.

Kakolanya alikuwa mwiba katika safu ya ushambuliaji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya kutofungana.

Safu kali ya ushambuliaji ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, ilikumbana na

safu imara ya ulinzi ya Yanga. Historia inaonyesha mara ya mwisho miamba hii miwili ya soka la Tanzania kukutana Jumapili Septemba 30, ilikuwa 2001 na kumalizika kwa sare

ya bao 1-1 huku Joseph Kaniki akiifungia Simba na Sekilojo Chambua akiisawazishia Yanga.

Miaka 17 baadaye, mashabiki wanashuhudia Simba na Yanga wakikutana tena Jumapili Septemba 30 na kushindwa kupatikana mbabe.

Nyota wa mchezo wa jana alikuwa ni kipa wa Yanga, Beno Kakolanya, ambaye kocha wake, Mwinyi Zahera, alimpanga badala ya Klaus Kindoki na hakuwaangusha mashabiki baada ya kupangua nafasi nyingi za wazi za Simba kupata mabao.

Matokeo ya jana katika mchezo uliohudhuriwa na maelfu ya mashabiki unazidi kuwafanya Mbao FC

kuendelea kukaa kileleni mwa ligi hiyo yenye timu 20, kwa kujikusanyia pointi 14 huku Yanga ikiwa katika nafasi ya pili na pointi 13 sawa na Mtibwa Sugar lakini wanao uwiano mzuri wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Simba wapo katika nafasi ya tano wakiwa na pointi 11 nyuma ya Azam FC ambao wanao pointi 12 na leo katika uwanja wao uliopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wataikabili Tanzania Prisons.

Kipa Kakolanya ambaye msimu uliopita hakupata nafasi na kufikia kususa kuichezea Yanga kutokana na

kile kilichodaiwa kuidai timu hiyo fedha zake za usajili, ameanza msimu huu vizuri na jana amedhihirisha ubora wake langoni.

Yanga walianza vizuri mchezo wa jana na dakika ya saba, beki wa kushoto, Gardiel Michael, alishindwa kutumia vyema pasi nzuri ya Heritier Makambo na kushuhudia shuti lake likipaa juu ya lango la Simba.

Simba ilicharuka na dakika nne baadaye, mshambuliaji raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, alipokea pasi ya Claotus Chama na kufumua shuti lililopanguliwa na Kakolanya.

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya Bingwa Leo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -