Friday, October 30, 2020

Zahera aenda kwao, aacha programu maalumu

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI


BAADA ya kufanikiwa kuwabana mahasimu wao, Simba, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, anatarajia kuondoka leo kwenda kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo.

Yanga juzi iliwabana Wekundu wa Msimbazi kwa kulazimisha suluhu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Zahera ni kocha msaidizi wa kikosi hicho kinachojiandaa na mechi ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika dhidi ya Zimbabwe, utakaochezwa Oktoba 13, mwaka huu, Kinshasa.

Akizungumza na BINGWA jana, Zahera alisema anatarajia kuondoka lakini kuna programu atamwachia kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila, ili kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Alisema bado anahitaji kuwaweka fiti wachezaji wake, hivyo wale ambao hawatakwenda katika timu zao za Taifa wataendelea na mazoezi kama kawaida kwa sababu mechi zilizopo mbele yao ni ngumu.

“Hakuna muda wa kupumzika, naondoka lakini nitaacha programu kwa zile siku ambazo sitakuwepo, kocha msaidizi ataendelea na mazoezi, kila mchezaji lazima afike mazoezini kwa wakati bila kutega,” alisema kocha huyo.

Programu anazoacha Zahera anapoondoka zimeonekana kuwa na mafanikio, kwani awali aliondoka baada ya mechi ya Yanga ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports nchini Rwanda na kufanikiwa kushinda mechi zote za ligi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -