Thursday, October 29, 2020

ZAHERA: OLE WAO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WIFRIDA MTOI


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewachimba mkwara wachezaji kwa kusema ole wake atakayetega mazoezi kwa kipindi ambacho hayupo, kwani hatampa nafasi katika kikosi chake hata awe na jina kubwa kiasi gani.

Zahera ameondoka juzi nchini kwenda kwao, DR Congo, kujiunga na timu yao ya Taifa inayojiandaa kucheza na Zimbabwe, jijini Kinshasa katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019), zitakazochezwa Cameroon mwakani.

Yanga tayari imecheza mechi tano za Ligi Kuu Tanzania Bara na kushinda nne, huku ikipata suluhu moja dhidi ya Simba, mchezo ulipigwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana kabla ya kuondoka nchini, Zahera alisema amemwachia msaidizi wake, Noel Mwandila, programu iliyoanza juzi hadi Oktoba 16 atakaporejea, lakini sharti kubwa aliloliacha ni kila mchezaji kuzingatia mazoezi.

Alisema akiwa kwao, atakuwa akifuatilia mwenendo wa wachezaji wote na uhudhuriaji wao mazoezi na mchezaji atakayebainika anategea, atamwambia Mwandila asimpange katika mechi zao zijazo.

“Ninaondoka, nakwenda timu ya Taifa ya Congo lakini nimeacha programu ya mazoezi yote kulingana na udhaifu ulioonekana katika mechi za nyuma, itafanyika kila siku hadi Oktoba 16, ninachotaka ni kila mchezaji kufika mazoezini bila visingizio.

“Kama kawaida yangu, nitakuwa nafuatilia programu inavyokwenda, mchezaji mvivu na anayetega mazoezini hatacheza mechi hata ikiwa ni ya kirafiki, nitaangalia wale wanaojituma tu,” alisema Zahera.

Kocha huyo alieleza kuwa anafahamu ratiba ngumu ya michezo iliyopo mbele yao na baadhi ya wachezaji wapo timu ya Taifa, hivyo lazima waliopo wazingatie kile kinachoelekezwa na mwalimu.

Tangu ametua Yanga, Zahera amejitambulisha kama kocha anayezingatia mno nidhamu ya wachezaji, akiwa amewahenyesha mastaa kibao wa timu hiyo waliokuwa ‘wakimzingua’.

Wakati Yanga ilipokuwa imeweka kambi Morogoro kujiandaa na msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Zahera alionyesha makucha yake kwa kumkimbiza Ibrahim Ajib uwanja mzima kwa siku tano baada ya straika huyo kuchelewa kuripoti kambini.

Mbali ya Ajib, staa mwingine wa Yanga aliyekiona cha moto kwa Zahera ni beki wa kulia, Juma Abdul ambaye kuna siku alitegea mazoezi ya asubuhi kwa madai ya kuumwa na tumbo, matokeo yake jioni akiwa amejiandaa kujumuika na wenzake, kocha huyo alimtaka kukimbia kuzunguka uwanja kwa takribani saa mbili kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, mjini humo.

Juu ya msimamo wake huo, Zahera aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya kuwasaidia wachezaji wasiojifahamu, akisisitiza kuendelea kuwahenyesha wavivu hata kama watakuwa ni mastaa kiasi gani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -