Wednesday, October 28, 2020

YANGA YAMWEKEA KIKAO KIZITO DJUMA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAITUNI KIBWANA

Baadaya kutimuliwa kwa Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, kwa sasa wapenzi wa soka wanasubiri kuona ama kusikia Mrundi huyo anatua timu gani. Kwa kuwa moja ya timu zinazotajwa kumwania, ipo Yanga, kocha huyo alipoulizwa juu ya Wanajangwani hao, alijibu: “Mambo ni ‘fire’ (moto).”

BINGWA ndilo lililokuwa gazeti la kwanza kuanika rasmi mpango wa Djuma kutemwa na Simba katika toleo la Jumamosi kwa kichwa cha habari, ‘Djuma yametimia’, baada ya kupenyezewa habari na mmoja wa vigogo wa Wekundu wa Msimbazi hao kuwa wameamua kuachana na kocha huyo.

Na sasa Djuma anasubiri kulipwa mamilioni yake ya kuvunjwa kwa mkataba wake ili aweze kurejea kwao Rwanda akisubiri ofa kutoka kwingineko, wakiwamo Yanga wanaotajwa kumpigia hesabu kwa muda mrefu.

Viongozi wa klabu ya Yanga, jana walifanya kikao kizito kumjadili Djuma, ili kuitumikia klabu hiyo kongwe nchini.

Yanga iliyochini ya Kocha Mkongo Mwinyi Zahera, mpaka msimu huu wa Ligi haijapata kocha msaidizi zaidi ya uwepo wa Mtaalam wa viungo Mzambia Noel Mwandila ambaye kwa sasa anatumika kama msaidizi.

Habari za uhakika pasipo na chembe ya uongo zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam, zilidai kuwa viongozi hao walimjadili Djuma kwa mapana na marefu na kuona anafaa kujiunga na Wanajangwani hao.

“Kwa kauli moja tumeamua kuanza mipango ya kumchukua Djuma asaidiane na Zahera, kwa sasa kocha wetu hana msaidizi na mambo yanakwenda akiongezeka huyu Mrundi tutakua vizuri zaidi,” alisema mpasha habari wetu.

Baada ya kumaliza kikao hicho Yanga walitafuta namba ya simu ya Djuma na kufanya nae kikao cha siri, ambapo inadawa kuwa Djuma aliridhia kwenda Yanga.

Akizungumza na BINGWA jana, Djuma ambaye juzi hakukaa katika benchi wakati wa mchezo wa Simba na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, alisema: “Wao ndio wamevunja mkataba wangu, si mimi na wamenipa barua. Mkataba wangu unaisha Oktoba mwakani.”

Djuma aliyewahi kuwa kocha bora Ligi ya Rwanda mwaka 2016, alipoulizwa iwapo ana mpango wa kujiunga na Yanga, alicheka na kujibu kiufupi: “Mambo ni fire (moto)”.

Kocha huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba, alisema kabla ya kuondoka nchini, amepanga kuwaaga wachezaji wa timu hiyo aliokaa nao vizuri tangu amejiunga na kikosi hicho.

“Nimepanga kuwaaga wachezaji, nilikuwa nao toka Oktoba mwaka jana, ila kama nitaruhusiwa kwa kuwa kila sehemu ina utaratibu wake,” alisema.

Djuma ametimuliwa Simba kwa madai ya kuingia katika migogoro na makocha wakuu wa klabu hiyo, kuanzia aliyepita, Mfaransa Pierre Lechantre hadi huyu wa sasa, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji.

Kocha huyo alianza kufanya kazi chini ya Mcameroon, Joseph Omog ambaye naye alifungashiwa virago Desemba mwaka jana, baada ya Simba kuondolewa kwa mikwaju ya penalti na Green Warriors ya Mwenge, Dar es Salaam katika michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania (FA).

Siku chache baada ya Omog kutimuliwa, Djuma akapewa mikoba ya kuisimamia Simba kama kaimu kocha mkuu na kibarua chake cha kwanza kilikuwa ni Kombe la Mapinduzi Zanzibar ambako walitolewa hatua ya makundi na Azam FC.

Baada ya michuano hiyo, Djuma akaletewa Lechante Januari mwaka huu, ambaye aliiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara waliousotea kwa takribani misimu mitano bila mafanikio.

Hata hivyo, Lechante alidumu ndani ya klabu hiyo kwa miezi mitano tu kabla ya Juni mwaka huu kuondoka, baada ya kile kilichoelezwa kutoelewana na Djuma, ndipo alipoletwa Aussems.

Lakini wakati Djuma akionekana kuitamani Yanga, Kocha Mkuu wa Wanajangwani hao, Mwinyi Zahera, amesema hamfahamu vizuri Mrundi huyo.

“Sifahamu utendaji kazi wake, hivyo siwezi kufanya kazi na mtu nisiyemfahamu vizuri,” alisema Zahera alipoulizwa juu ya uwezekano wa kufanya kazi na Djuma.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -