Monday, October 26, 2020

ZAHERA AJA NA ‘SURPRISE’ YANGA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka bayana kuwa anatarajia kuleta vifaa vipya katika kikosi hicho kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo na kuna uwezekano akaja nao kesho akitokea Zimbabwe.

Zahera yupo katika kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo, kilichopo nchini Zimbabwe na kinatarajia kushuka dimbani leo kucheza mchezo wao wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) zitakazopigwa nchini Cameroon mwakani.

Mchezo huo wa marudiano utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe baada ya ule wa awali kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Akizungumza na BINGWA jana kwa simu kutoka Zimbabwe, Zahera, alisema kuna wachezaji ambao anawafuatilia na wamefikia pazuri huenda akaja nao baada ya kumaliza mechi yake na Zimbabwe.

Kocha huyo hakupenda kutaja majina ya wachezaji hao, nchi wanayotokea na nafasi zao kwa kusema bado ni mapema kuwaweka wazi hadi pale watakapofika nchini.

“Mungu akipenda kuna wachezaji nitakuja nao kwa ajili ya kuimarisha kikosi changu kuelekea mbio za ubingwa, ila itakuwa ni ‘surprise’ kwa wapenzi wa Yanga sitaki kuwataja sasa hivi, nikifanikiwa kuja nao mtawaona,” alisema.

Alisema anatarajia kurejea nchini kesho akiwa na wachezaji hao kama watakuwa wamekamilisha taratibu za kusafiri.

Zahera alisema ataondoka Zimbabwe baada ya mchezo huo ili kuwahi mechi ya Yanga na Alliance, inayotarajia kupigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga licha ya kutopoteza mechi kati ya sita za Ligi Kuu Tanzania Bara walizocheza, bado kinaonekana kinahitaji kuimarishwa zaidi hasa katika safu ya ushambuliaji na kiungo.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Yanga ipo nafasi ya tatu na pointi 16 zilitokana na michezo sita baada ya kushinda mitano na kutoka sare mmoja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -