Saturday, October 31, 2020

RAMOS AMVUTA KANE LA LIGA KIAINA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MADRID, Hispania

NAHODHA wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Hispania, Sergio Ramos, ni kama amemvuta kiaina staa wa Tottenham, Harry Kane, baada ya kusema kwamba anavyoamini ana uwezo wa kufanya makubwa katika michuano ya La Liga.

Kauli ya staa huyo imekuja baada ya mshindi wa kiatu cha dhahabu mara mbili katika michuano ya Ligi Kuu England katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni kuwa akihusishwa kujiunga na mabingwa hao wa Ulaya.

Msimu huu pia Kane ameshaifungia Tottenham mabao matano katika michuano ya Ligi Kuu England na   Ramos alimmwagia sifa kabla ya mechi yao ya jana ya timu za Taifa iliyotarajiwa kupigwa mjini Seville.

Akizungumza juzi wakati alipohojiwa kuhusu uwezo wa timu ya Taifa ya  England na mchezaji ambaye anaweza kupata mafanikio nchini Hispania, Ramos, alisema kwamba kwa ujumla ni wachezaji wote, lakini akamsifia zaidi Kane.

“Ni kweli kwamba kitu ambacho kinafurahisha katika Ligi Kuu England ni nguvu, lakini wachezaji wana kila aina ya ubora,” alisema staa huyo.

“Harry Kane, ni mmoja wa mfano kutokana na uwezo wake wa ushambuliaji na vile vile uwezo wake ambao unawaduwaza kila beki, lakini kwangu sitaki iwe hivyo,” aliongeza beki huyo mtata.

Alisema kuwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya England kuna mastraika wengine wengi ambao ni hatari, lakini akasema kwamba anaweza kuwahakikishia mashabiki kwamba wameshawasoma vizuri na hawezi kufanya kitu.

 

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -