Friday, October 23, 2020

AMUNIKE: TANZANIA IMEBARIKIWA VIPAJI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA TIMA SIKILO

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, amesema kuwa, Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji lukuki vya soka, huku akiweka wazi matumaini yake ya kukiona kikosi chake kikifuzu fainali za Afcon 2019.

Stars juzi ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa fainali hizo za Kombe la Mataifa ya Afrika, uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA juzi, Amunike alisema kuwa, iwapo vipaji hivyo vitaaminiwa na kupewa nafasi, Tanzania itafika mbali.

Katika mchezo wao wa kwanza uliochezwa nchini Cape Verde wiki iliyopita, Stars ilichezea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao hao.

Mchezo unaofuata, Tanzania itarudiana na Lesotho Novemba 16, mwaka huu nchini Lesotho, ikiwa ni baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 Juni 11, mwaka jana kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Amunike alisema Watanzania, wanapaswa kufahamu kuwa, katika kila mchezo kuna kushinda na kushindwa, hivyo wasiwe rahisi kuondoa imani yao kwa wachezaji, kwani ili wafanye vizuri wanahitaji ushirikiano na kuendelea kuaminiwa.

Alisema ameangalia Tanzania na ameona kuna vijana wengi ambao wana uwezo mkubwa katika soka na kinachotakiwa ni kuwa na imani nao kuwa wana uwezo wa kufanya mazuri.

“Kila safari ina changamoto yake, kikubwa ambacho tunapaswa kufahamu ni kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na wachezaji wengi wazuri, kinachopaswa ni kuwaamini na kuwa pamoja nao,” alisema Amunike.

Alisema anakiamini kikosi chake na anaamini nidhamu na uwezo waliouonyesha katika mchezo wa juzi, wataiendeleza hata ndani ya klabu zao, Tanzania itakuwa na timu bora ya Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -