Tuesday, October 20, 2020

WAMEBOBEA Hawa kwa kutengeneza nafasi za mabao, hawana mpinzani

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England

WACHEZAJI wengi bora duniani hujulikana kwa vitu wanavyovifanya uwanjani ambavyo kimsingi huwa havitoshi kuelezewa mdomoni tu.

Iwe ni kufunga mabao kwa kiwango cha kutisha au kuokoa michomo ya hatari, yapo maeneo mengi ambayo hutengeneza wachezaji kadhaa wenye ubora wa kutukuka.

Na ndio maana ilianzishwa mifumo ya kukusanya data ili kuzisaidia hata klabu zinazohitaji wachezaji bora kutopata ugumu wa kuwatafuta.

Moja ya eneo muhimu katika timu ni kuwa na mchezaji mwenye uwezo wa kutengeneza nafasi za mabao.

Wachezaji wa namna hiyo wametokea katika vizazi tofauti vya soka na kuupamba mchezo huo katika kila kona ya dunia.

Julai mosi mwaka 2006, ulianzishwa mfumo wa Opta kwa lengo la kukusanya takwimu mbalimbali, ingawa ipo mingine tofauti ambayo imekuwa ikifanya hivyo pia.

Opta wametoa orodha ya wachezaji wenye wastani bora wa kutengeneza nafasi nyingi za mabao kwa dakika 90 barani Ulaya, tangu walipoanza kukusanya takwimu na majina yaliyopo kiukweli si ya mchezo mchezo.

Wachezaji hao wameorodheshwa na rekodi nyingine za jumla ya mechi walizocheza, dakika pamoja na asisti.

  1. Cristiano Ronaldo

Mechi: 401, Dakika: 34,107, Nafasi: 695, Asisti: 111

Zaidi ya uwezo wa kuzifumania nyavu alionao Ronaldo, pia Mreno huyo ni mtengenezaji mzuri sana wa nafasi za mabao.

Katika jumla ya nafasi 695 alizotengeneza hadi sasa ana wastani wa kutengeneza nafasi 2.33 kwa dakika 90.

  1. Marek Hamsik, Mechi: 400, Dakika: 30,952, Nafasi: 740, Asisti: 80

Mslovakia huyo ambaye ni mfungaji bora wa muda wote katika klabu ya Napoli, amekuwa katika kiwango cha hali ya juu kwa muda mrefu kwa muda wa miaka 12 sasa.

Ukiachana na aina yake ya unyoaji nywele ya ‘kijogoo’ kilichonyooka vilivyo, Hamsik pia ni mpigaji pasi za mwisho mzuri mno, akiwa na wastani wa kutengeneza nafasi 2.15 za mabao kwa dakika 90.

  1. Lionel Messi, Mechi: 402, Dakika: 33,213, Nafasi: 861, Asisti: 151

Ukiweka pembeni uwezo wa kuzifumania nyavu alionao ‘mchawi’ huyo wa soka, pia hata jukumu la kutengeneza nafasi za mabao analiweza kwa asilimia zote.

Kwa mujibu wa Opta, Messi anashikilia nafasi ya tano katika orodha ya waliotengeneza nafasi nyingi za mabao (861), lakini kwa wastani wa kutengeneza nafasi 2.33 kwa dakika 90, anashikilia nafasi ya nane.

Hata hivyo, Messi anaongoza kwa kutoa pasi nyingi za mabao (151).

  1. Juan Mata, Mechi: 355, Dakika: 25,960, Nafasi: 723, Asisti: 79

Kiungo huyo wa Hispania anayekubalika mno na mashabiki wa soka na yeye hajakosekana katika eneo hili la kutengeneza nafasi za mabao, akiwa na wastani wa 2.51 kwa dakika 90 tangu msimu wa 2006/2007.

Kinachomfanya Mata apendwe tangu akiwa Valencia kabla ya kuhamia Chelsea na Manchester Utd, ni soka lake la kiufundi zaidi na uwezo wa kufunga mabao ya faulo.

  1. Eden Hazard, Nafasi: 363, Dakika: 27,377, Nafasi: 794, Asisti: 77

Mfalme huyo wa kukokota mpira wa Stamford Bridge, Hazard, ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kusakata soka katika Ligi Kuu England.

Hoja hiyo inaongezewa nguvu na takwimu yake ya kuwa na wastani wa kutengeneza nafasi 2.61 kwa dakika 90 na hadi leo ameweza kutengeneza jumla ya nafasi 794 na kutoa pasi 77 za mabao.

  1. David Silva, Mechi: 374, Dakika: 29,604, Nafasi: 886, Asisti: 100

Bila ubishi, Silva ni mchezaji bora zaidi wa Man City, tangu vinara hao wa Ligi Kuu England waanze kumilikiwa na Waarabu.

Opta walipoanza kukusanya data, Silva alikuwa bado akisakata soka nchini Hispania na baada ya miaka 12, kiungo huyo anashikilia nafasi ya tano kwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao kwa wastani wa 2.69 kwa dakika 90.

  1. Cesc Fabregas, Mechi: 372, Dakika: 28,174, Nafasi: 932, Asisti: 133

Wanaomkubali zaidi kiungo huyo wamempachika jina la ‘Mkurugenzi wa ubunifu’. Umaarufu wa Fabregas ulitokana na pasi zake za uhakika kila anapoinua uso wake kutazama wapi straika alipo .

Tangu 2006 Mhispania huyo amekuwa na wastani bora wa kutengeneza nafasi 2.98 za mabao kwa dakika 90 na pia anashikilia rekodi ya Ligi Kuu England kwa kutoa pasi zaidi 15 za mabao akiwa na umri mdogo zaidi.

Na pia ni mchezaji pekee kutoa zaidi ya pasi 10 za mabao katika misimu sita tofauti ya ligi hiyo.

  1. Dimitri Payet, Mechi: 404, Dakika: 29,844, Nafasi: 1016, Asisti: 104

Najua umeshtuka kuliona jina la Mfaransa huyo, lakini takwimu zake zinaruhusu awepo hapa.

Tangu 2006, Payet ametengeneza jumla ya nafasi 1016 za mabao, licha ya kwamba hakuwahi kucheza katika klabu kubwa zaidi za Bara la Ulaya.

Uwezo wake mkubwa upo katika mipira iliyokufa na ni mmoja kati ya wachezaji watatu wenye wastani wa kutengeneza zaidi ya nafasi 3.00 (3.06) za mabao kwa dakika 90.

  1. Francesco Totti, Mechi: 284, Dakika: 20,405, Nafasi: 696, Asisti: 73

Gwiji huyo wa AS Roma aliyapendezesha maisha yake ya soka katika klabu moja tu kwa kufunga mabao makali na kuwatengenezea wenzake nafasi za kufanya hivyo pia.

Wakati Opta wanaanza shughuli zao, Totti ndio alikuwa anaelekea kufikisha umri wa miaka 30 na ndio kwanza alikuwa amecheza mechi nne tu za ligi akiwa na miaka 29 na tangu mwaka huo hadi anastaafu aliweza kuandikisha wastani wa kutengeneza nafasi 3.07 za mabao kwa dakika 90.

  1. Mesut Ozil, Mechi: 354, Dakika: 26,561, Nafasi: 1033, Asisti: 128

Kiungo mchezeshaji huyo wa Kijerumani ndiye anayeongoza kwa kutengeneza jumla ya nafasi nyingi za mabao (1033) tangu 2006 na wastani kwa dakika 90 (3.5). Nini kingine unachokitaka kutoka kwa Ozil?

Katika maisha yake yote ya soka amekuwa ni mchezaji wa kuwapikia wengine. Na katika kizazi chake, wengi wanapaswa kumheshimu kwa hilo.

Masuala mengine ya kukaba amewaachia akina Lucas Torreira.

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -