Friday, October 30, 2020

TSHABALALA AMTUMIA SALAMU KWASI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA TIMA SIKILO


BEKI wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, ameweka wazi kuwa kwa sasa wapinzani wake watulie, kwani amepanga kukaza zaidi ili kuendelea kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha timu yao.

Msimu uliopita katika mzunguko wa pili, Tshabalala hakupata nafasi nyingi ndani ya kikosi cha kwanza cha Simba kutokana na kuwapo kwa Mghana Asante Kwasi ambaye alisajiliwa kupitia dirisha dogo akitokea Lipuli ya Iringa.

Akizungumza na BINGWA jana, Tshabalala alisema anashukuru kupata nafasi ya kucheza msimu huu tofauti na uliopita ambao alikuwa akikabiliwa na wimbi la majeruhi.

Tashabalala alikiri kuwa kikosi chao cha kwanza kimekuwa na ushindani mkubwa wa namba, kwani kila mchezaji yuko vizuri, hivyo anahitaji kuonesha uwezo wake ili aendelee kupeta.

“Namshukuru Mungu msimu huu kwangu si mbaya kwa kuwa napata nafasi na nina maendeleo mazuri, najitahidi kupambana ili nisije nikaipoteza hii nafasi,” alisema.

Alisema siku zote timu inapofanya vizuri huku baadhi ya wachezaji wanakaa benchi, inakuwa ni mtihani kwani imani ya kupata nafasi inakuwa inazidi kupotea, hivyo anamwomba Mungu amsaidie ili asifanye vibaya na kupoteza namba yake.

Juu ya anavyoiona Ligi Kuu Bara msimu huu, alisema kuna changamoto kubwa tofauti na msimu uliopita, hali hiyo ikizikabili timu zote na si Simba pekee.

“Ligi ya msimu huu imekuwa na changamoto kwani kila timu imekuwa na mapitio yake, lakini tutapambana kufanya vizuri,” alisema.

Japo hajamtaja Kwasi, lakini kauli ya Tashabalala huenda zikawa ni salamu tosha kwa mwenzake huyo kupambana hasa ili kupata nafasi katika kikosi cha Kocha Mkuu, Mbelgiji Patrick Aussems.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -