Saturday, October 31, 2020

JPM akutana na Timu ya Taifa, aahidi milioni 50

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Na Lulu Ringo  

Timu ya Taifa (Taifa Stars), imepata fursa ya kupata chakula cha mchana na Rais John Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam ambaye pamoja na mambo mengine amewapongeza na kuwapa hamasa wachezaji hao kufanya vizuri katika mashindano ya kusaka tiketi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa Huru Barani Afrika (AFCON) nchini Cameroon mwakani.

Hafla iliyofanyika leo Ijumaa Oktoba 19, imekua ya neema kwa vijana hao wa Stars baada ya Rais Magufuli kutoa ahadi ya kuwapatia fedha taslimu Sh milioni 50, ili iwasaidie katika mchakato wa kuwania nafasi hiyo ya kushiriki AFCON mwakati ambapo mara ya mwisho Tanzania ilifuzu michuano hiyo, mwaka 1980.

“Katika mkakati huu nitawaongezea Sh milioni 50 na zitumike kweli kwa watu wanaotakiwa, kwa sababu unaweza kukuta wachezaji wanaokwenda kucheza ni 15 lakini viongozi wanakuwa 30 nao wanataka kusafiri na timu, ni lazima tuiache timu iende na watu wanaotakiwa ili hata wachezaji wapate posho ya kutosha,” amesema Rais Magufuli.

Aidha, hafla hiyo pia imehudhuriwa na baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ambaye amesema katika mikakati ya kuhakikisha wanaunga mkono soka la Tanzania wameanzisha bahati nasibu inayoitwa Sport Betting.

“Tumeanzisha Sports Betting ambayo imetokana na mabadiliko ya sheria ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ambapo awali sheria ya michezo ya kubahatisha haikutambulika hapa nchini lakini sasa nchi yetu nayo inaendesha michezo hii ya kubahatisha,” amesema Dk. Mwakyembe.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na baadhi ya viongozi akiwamo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, Kocha wa Stars Emanuel Amunike, Mwenyekiti wa BMT, Leodgar Tenga.

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -