Friday, October 23, 2020

TANZANITE YAFUNGUA PAZIA LA LIGI KUU ARUSHA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA GLORY MLAY

Pazia  la Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara linatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni na litashirikisha timu 12, huku michezo ikichezwa mtindo wa nyumbani na ugenini kwenye viwanja mbalimbali hapa nchini.

Timu shiriki katika ligi hii ni pamoja na Simba Queens, Yanga Princess, JKT Queens, Evergreen (Dar es Salaam), Baobab ya Dodoma, Sisterz ya Kigoma, Mlandizi Queens (Pwani) na Alliance Girls (Mwanza).

Ligi hiyo itaanza kwa makundi na kufuata hatua ya nane bora, ambapo timu mbili zilizopata matokeo yasiyoridhisha zinashuka kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Tanzanite Queens ndio timu pekee mkoani Arusha inayoshiriki Ligi Kuu kwa upande wa wanawake Tanzania Bara, kwani hapo awali kulikuwa hakuna timu ya wanawake ya klabu hiyo ambayo imeanzia katika ngazi ya mkoa na hatimaye kufanikiwa kuwa mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza.

Kupanda kwa timu hiyo kumewapa changamoto viongozi wa michezo mkoani hapo, kwani hakuna timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu kwa wanaume bali nyingi zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza, ikiwamo Arusha United na Arusha FC.

BINGWA lilipata nafasi ya kufanya mazungumzo na kocha mkuu wa timu hiyo, Adballah Juma, kuhusu suala zima la maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu.

MAANDALIZI

Anasema wanatarajia kuanza kambi mapema kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi hiyo, huu ni wakati mwafaka sasa kukiona kikosi chake katika mechi za kirafiki.

“Tumejipanga vyema kufanya maandalizi ya kutosha, hivyo hatuna hofu yoyote katika msimu huu wa ligi, tunachohitaji ni sapoti  kutoka kwa wadau ili kuweza kujijengea mazingira mazuri ya ushindi katika mechi tutakazocheza.

“Hatuna majeruhi wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi wapo katika hali nzuri, hivyo tunachosubiri ligi ianze tuanze kukusanya pointi tatu mapema kwa kila mchezo tutakaocheza,” alisema Juma.

Alisema ligi itakuwa ngumu kwani kila timu imejipanga kwa nafasi yake, huku akidai kuwa watazichukulia kwa uzito mechi zote watakazocheza.

Mechi dhidi ya Simba, Yanga

Juma anasema kwamba watahakikisha wanashinda katika mchezo wao huo ikiwemo ya Simba na Yanga, ili kuwapa raha mashabiki wao kwani wanaamni hizo ni timu kubwa hivyo wakizifunga watazidi kujipa jina.

Alisema watakapoingia kambini watafanya  maandalizi ya kutosha, watatumia nafasi ya kuonyesha kile watakachokipata kutoka katika kambi kwa mashabiki wao kwa kizifunga timu hizo.

“Pointi tatu kwetu lazima, tunataka kuanza ligi vizuri ili kujirahisishia kazi ya kuwa mabingwa msimu huu, kila mchezaji anatakiwa kujituma kwa kadiri ya uwezo wake ili kuiletea timu mafanikio,” anasema Juma.

Alisema kikosi chake kipo imara, hivyo aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi pindi watakapocheza kushuhudia timu yao ikichukua pointi tatu kwa Simba na Yanga.

“Ni mechi ngumu ila tunauwezo wa kushinda, tutacheza soka la kujituma na kupambana zaidi,” anasema Juma.

MIKAKATI YAO

Juma amesema wanahitaji kufumua kikosi kizima na kusajili wachezaji 10 ambao watasaidia kuweka sawa sehemu zilizokuwa na mapungufu katika kikosi hicho.

Anasema kikosi chake kilionyesha mapungufu makubwa, wataongeza wachezaji hao ili kukiimarisha kukabiliana na timu za ligi hiyo.

Hata hivyo, amekiangalia kwa umakini kikosi na kugundua kuwa kuna baadhi ya mapungufu na kuona kuwa kati ya wachezaji hao wanaohitajika ni mabeki wanne, washambuliaji wawili, makipa wawili na viungo wawili.

“Ligi Kuu msimu uliopita tumeiona na tumeifuatilia, kuna timu ambazo zipo vizuri kama JKT Queens, Simba na Yanga pia hivyo basi lazima tujipange vilivyo, tunahitaji kuongeza wachezaji hao kwani mapungufu yalikuwepo mengi,” anasema Juma.

MATARAJIO

Mashabiki wanatakiwa kuungana kwa pamoja na timu hiyo ili kuleta maendeleo makubwa msimu huu.

Alisema endapo wataungana kwa pamoja wataweza kuchukua ubingwa msimu huu, hivyo wadau na wapenzi wa timu hiyo waelekeze nguvu katika harakati za kusaka ubingwa.

“Matarajio yetu ni makubwa kwa mashabiki endapo tutaungana bega kwa bega, tunatamani kuona msimu huu wa mabadiliko kwani ligi hii haina mwenyewe, hivyo timu yoyote inaweza kuwa bingwa.

“Ninachowaomba mashabiki na viongozi tushikamane, tuwe na umoja ili kufanikisha timu hii kushinda michezo yake pale itakapokuwa ikicheza haijalishi na timu gani inacheza nayo,” anasema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -