Sunday, November 1, 2020

KLABU ZISAKE UDHAMINI KUONGEZA USHINDANI WA SOKA LIGI KUU BARA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

WAKATI Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa katika mzunguko wa 10, baadhi ya klabu zimeonekana kushindwa kuhimili uendeshaji wa timu zao kutokana na kukabiliwa na ukata.

Msimu huu Ligi Kuu inaendeshwa bila mdhamini mkuu baada ya Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, kushindwa kuongoeza mkataba mpya.

Mdhamini huyo aliyedumu zaidi ya misimu mitano, wakati huu klabu zinabeba mzigo mkubwa wa kutafuta fedha kwa ajili ya kuandaa timu zao, tofauti na misimu mingine zilikuwa zinapata mgao kutoka sehemu ya udhamini wa Vodacom.

Kukosekana kwa mdhamini mkuu katika msimu huu kumezifanya baadhi ya timu zishindwe kujiendesha, lakini pia kuandaa kikosi bora.

Hivi karibuni timu ya Ndanda ilishindwa kusafiri kutoka mkoani  Singida na kurejea Mtwara kutokana na kukabiliwa na ukata.

Lakini timu ambazo hazina uchumi mkubwa kama Lipuli, African Lyon, Alliance, Biashara United na nyinginezo, itakuwa ni vigumu kuonyesha kandanda safi kutokana na kutokuwa na fedha za kuandaa timu yenye ushindani.

Tunasema kwamba, kukosekana kwa udhamini katika timu hizo kutasababisha kukosa ushindani wa kweli Ligi Kuu msimu huu.

BINGWA tunasema kwamba ligi ya msimu huu inaweza kuwa ya timu tano zenye uchumi mkubwa, huku nyingine zikionyesha kushindwa kuonyesha ushindani kutokana na kukosa fedha za kujiendesha.

Pamoja na Vodacom kushindwa kuongeza mkataba mpya kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), bado kuna nafasi kwa klabu kutafuta wadhamini wao ambao watasaidia kuendeleza timu zao.

Tunaamini kwamba, klabu zinaweza kupata udhamini kutoka kwa makampuni mbalimbali nchini kama ilivyo kwa timu za Simba, Yanga, Singida United na nyinginezo.

BINGWA tunasema klabu ambazo hazina udhamini zianze kuweka mkakati wa kujiendesha kwenye ligi hiyo.

Kwa upande wetu tunaamini kwamba, ushindani wa ligi utawezesha kupata bingwa bora ambaye anaiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa mwakani.

Tunasema kwamba ni wakati wa klabu za Ligi Kuu kuongeza ubunifu wa kuendesha timu zao kuliko kuendelea kutegemea ufadhili.

 

 

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -