Tuesday, October 20, 2020

UKIKUTANA NA SIMBA, UNAKUFA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI


MSHAMBULIAJI wa Uganda, Emmanuel Okwi ameendeleza moto wake, baada kuisaidia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 akipiga ‘hat-trick’ yake ya kwanza msimu huu.

Simba waliibuka na ushindi huo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting ya Mlandizi, uliopigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Simba wamepanda hadi nafasi ya pili wakijikusanyia jumla ya pointi 23 baada ya michezo yao 10 wakiachwa kwa pointi nne na Azam FC.

Mchezo huo uliaanza kwa kasi na dakika ya saba iliwatosha Wekundu hao wa Msimbazi kuandika bao la kwanza lililofungwa na Okwi akitumia vizuri pasi ya Shomari Kapombe iliyokolewa vibaya na mabeki wa Ruvu.

Ruvu walijaribu kusawazisha dakika ya 16 kupitia Said Dilunga, lakini alipiga shuti lililopaa juu ya lango la Simba.

Simba waliendelea na kasi yao na dakika ya 23 waliongeza bao la pili lililofungwa na Meddie Kagere, baada ya krosi ya Shiza Kichuya kumkuta Okwi aliyegongesha mwamba na mpira kukwamishwa wavuni na mfungaji huyo.

Mchezo huo ulitawaliwa na Simba, ambapo dakika ya

30, Kapombe alipoteza nafasi ya wazi baada ya kupiga shuti lililopaa juu ya lango la Ruvu, kabla ya ya dakika nne baadaye naye Kagere kupoteza nafasi nyingine.

Okwi angeweza kuifunga Ruvu mabao manne kama msimu uliopita, baada ya kutingisha nyavu akiwa kwenye eneo la kuotea na hadi mapumziko Simba walikuwa wakiongoza kwa mabao hayo mawili.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Kagere kupoteza nafasi ya wazi kwa kupaisha mpira aliyotengewa na John Bocco.

Dakika mbili baadaye beki wa kati wa Simba, Jjuuko Murshid alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi wa Amada Simba kutoka Kagera kwa kumfanyia madhambi Dilunga.

Okwi aliifungia Simba bao la tatu dakika ya 53 akitumia tena krosi ya Kapombe na dakika ya 67 kocha wa Simba, Patrick Aussems alifanya mabadiliko kwa kumtoa Kagere na kuingia Hassan Dilunga, huku Ruvu wakimpumzisha Full Maganga na kuingia Alinanuswe Martine.

Bocco alipoteza nafasi nyingine dakika ya 75 kwa shuti lake kwenda pembeni ya lango la Ruvu akiwa ndani ya boksi dogo baada ya kuwekewa mpira mzuri na Kapombe.

Kinara wa mabao msimu uliopita, Okwi alikamilisha ‘hat-trick’ yake dakika ya 77 akitumia akitengewa tena na Kapombe aliyepiga krosi na Bocco kuushindwa mpira huo na kumkuta nyota huyo wa Uganda.

Okwi alikosa bao lingine dakika 80 kwa kupiga nje ya lango la Ruvu na dakika nne baadaye alipumzishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Salamba, ambaye alifunga karamu ya mabao kwenye mchezo huo uliomalizika kwa mabao 5-0 kwa kupachika bao hilo la mwisho.

Kwasasa Okwi atakuwa amemfikia kinara wa mabao Eliud Ambokile wa Mbeya City wote wakiwa na mabao saba katika orodha ya wafungaji.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -