Sunday, October 25, 2020

SAMATTA ASAKA KIATU CHA DHAHABU UBELGIJI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

BRUSELLS, Ubelgiji


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania na timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, ameendeleza moto wake wa kufunga mabao, akionesha wazi kuwa anakitaka kiatu cha dhahabu kwenye Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu.

Samatta alifunga bao moja kwenye mchezo wa ligi hiyo dhidi ya Standard Liege, mtanange ambao ulimalizika kwa timu hizo kugawana pointi moja kufuatia sare ya bao 1-1.

Hilo ni bao la nane kwa Samatta msimu huu, likimfanikisha kukwea hadi nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi hiyo sambamba na Landry Dimatta wa Anderlecht, mwenye idadi kama hiyo.

Hata hivyo, kazi inaweza kuwa kubwa kwa Samatta kwani wanaowafuatia yeye na Dimatta kwa kufunga mabao mengi kwenye Ligi Kuu Ubelgiji, msimu huu ni Ivan Santini wa Anderlecht na Leandro Trossard wa Genk.

Mastraika hao wawili wote wana mabao nane, hivyo kuufanya mchuano wa kuwania kiatu cha dhahabu kuwa mkali na wa kusisimua.

Samatta alicheka na nyavu kwa mara nyingine tena siku chache baada ya kumtungua mabao mawili kipa wa Liverpool, Loris Karius, anayecheza kwa mkopo Besiktas ya Uturuki, kwenye mechi ya Ligi ya Europa.

Kiwango hicho cha Samatta kiliisaidia Genk kuibamiza Besiktas mabao 4-2 na kuondoka ugenini na pointi tatu muhimu, zilizowapandisha hadi nafasi ya kwanza kwenye kundi lao.

Hadi sasa Samatta ameshaifungia Genk jumla ya mabao 16 katika michuano yote msimu huu, akivuka idadi ya mabao 15 aliyoifungia Genk katika michuano yote ya msimu wa 2016/17.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -