Monday, October 26, 2020

KARIHE APANIA KUWATIBULIA YANGA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA WINFRIDA MTOI


STRAIKA wa timu ya Lipuli FC, Seif Abdallah ‘Karihe’, amepania kuwatibulia Yanga katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Karihe ambaye msimu uliopita alifunga bao lililoifanya Lipuli kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru, aliliambia  BINGWA kuwa wamejipanga kuhakikisha timu yao inaondoka na pointi tatu na kutibua rekodi ya kutofungwa kwa Wanajangwani hao.

Aidha, alisema tangu ligi hiyo imeanza  hajafanikiwa kufunga bao hata moja, lakini  huenda akaanza kwa kutikisa nyavu za Yanga kama alivyofanya msimu uliopita.

“Tumetoka kushinda dhidi ya Mbao, lakini pia wachezaji tumejipanga kuendeleza kasi yetu ili kuchukua pointi ugenini, najua haitakuwa mechi rahisi lakini tutapambana,” alisema Karihe.

Hata hivyo, Karie alikiri kwamba haitakuwa kazi rahisi kwao kupata matokeo mazuri mbele ya Yanga kwa sababu kikosi chao kimebadilika kila idara na si kama kilivyokuwa msimu uliopita.

“Kikosi cha Yanga msimu huu ni imara hivyo si rahisi kuwafunga, inahitaji ujipange sawa sawa maana ukiangalia hawajapoteza mchezo hata mmoja tangu wameanza Ligi Kuu,” alisema.

Hadi sasa Yanga imejikusanyia pointi 22 baada ya kucheza michezo nane, ambapo imeshinda saba na kutoka sare mara moja, huku Lipuli wakiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 10, wakishinda mbili, sare sita na kupoteza mbili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -