Monday, October 26, 2020

MFAUME APIGWA KWA TKO URUSI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ZAITUNI KIBWANA


BONDIA Mtanzania, Mfaume Mfaume, juzi alichezea kichapo baada ya kupigwa kwa TKO  katika raundi ya pili hivyo kupoteza pambano lake la ubingwa wa dunia uzito wa kati dhidi ya mpinzani wake, Vaghinak Tamrazyan, lililopigwa nchini Urusi.

Mfaume aliyekuwa akipigana katika uzito wa Kg 66, hakuweza kufurukuta dhidi ya mpinzani wake na kujikuta akiambulia ngumi nzito zilizomfanya ashindwe kuendelea na pambano.

Akizungumza na waandishi wa habari, wakala wa bondia huyo, Jay Msangi, alisema kichapo cha Mfaume kimetokana na waamuzi kushindwa kusimamia sheria za mchezo.

“Matokeo hayakuwa halali kwa kuwa mwamuzi hakutenda haki maana alimaliza pambano wakati Mfaume alikuwa tayari kuendelea licha ya kuhesabiwa muda,” alisema.

Msangi alisema tukio hilo la mwamuzi liliwahuzunisha mashabiki waliofika ukumbini na kumfanya Mfaume amwage machozi akiwa ulingoni kwa machungu.

“Sina la kusema ila tumepoteza pambano mapema sana, lakini kwa mshtuko mkubwa mwamuzi aliamua kumaliza pambano licha ya wadau kushangazwa wakiwa haelewi nini kimetokea,” alisema Msangi.

Aidha, Msangi aliongeza kuwa Mfaume anatarajia kurejea nchini leo na baada ya kuwasili atazungumza na waandishi wa habari.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -