Thursday, October 29, 2020

PAMBA YAPAA KILELENI FDL

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA DAMIAN MASYENENE, MWANZA


MAMBO yamenoga kwa timu ya Pamba ya jijini Mwanza inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), baada ya kushinda mchezo wake wa tatu mfululizo na kujikita kileleni mwa Kundi B.

Katika mchezo uliopigwa juzi Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, Wana TP Lindanda Pamba SC, waliichapa Mgambo Shooting ya Tabora 3-0 mabao yaliyofungwa na Ally Athuman dakika ya 10, la pili likipatikana baada ya beki wa Mgambo, Christian Mazula, kujifunga dakika ya 21, wakati la tatu likikwamishwa nyavuni na Kelvin John dakika ya 31.

Ushindi huo unawafanya Pamba kujikita kileleni na pointi tisa wakifuatiwa na Geita Gold yenye pointi nane wakiwaacha Arusha United na Dodoma FC waliopoteza michezo yao ya juzi.

Baada ya ushindi huo wa tatu mfululizo, kocha mkuu wa Pamba, Juma Yusuph ‘Sumbu’, alisema matokeo hayo mazuri yanazidi kuwapa imani na kujiamini akisisitiza malengo yao ya kurejea Ligi Kuu Bara.

“Vijana wangu bado hawajawa makini kwa sababu tunaendelea kupoteza nafasi za kufunga, licha ya timu kucheza vyema ukizingatia tulichelewa kuanza maandalizi,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -