Monday, October 26, 2020

HAKUNA HAJA YA KUMUOTA STEWART HALL

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA OSCAR OSCAR

KAMA kuna kosa kubwa ambalo Real Madrid waliwahi kulifanya katika siku za hivi karibuni, ilikuwa ni hili la kumuuza Mesut Ozil kwenda Arsenal. Kama kuna kosa jingine kubwa alilofanya Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, basi ni kumtimua kazi kocha Carlo Ancelotti.

Soka ni mchezo wa makosa, Real Madrid hawawezi kulikwepa kosa hili pamoja na kuwa kocha wa sasa, Zinedine Zidane, anafanya vizuri. Moja kati ya makosa makubwa ambayo kocha, Louis Van Gaal, aliwahi kuyafanya akiwa na Manchester United ni kumuuza Angel Di Maria kwenda PSG.

Azam FC kwa hapa kwetu bado wanaonekana kusuasua, lakini moja kati ya makosa makubwa waliyoyafanya hivi karibuni ni kuachana na kocha wao, Joseph Marious Omog, ambaye kwa sasa yupo na Wekundu wa Msimbazi, Klabu ya Simba.

Makosa ni sehemu ya mchezo wa soka, ni vigumu kuyaepuka. Pamoja na uwekezaji mkubwa unaofanywa na wamiliki wa klabu ya Azam, bado timu hiyo inaonekana kusuasua kunako ligi kuu Tanzania bara. Kichapo dhidi ya Simba na Ndanda FC, ni ngumu kumeza kwa wamiliki wa klabu hiyo.

Bado Azam wanapaswa kuwa watulivu na kumwamini kocha wao raia wa Hispania, Hernandez. Kichapo dhidi ya Simba kinaweza kubebeka kirahisi kwa sababu Simba ni moja kati ya timu bora kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Huu utamaduni wa Ndanda FC kuendelea kujichotea pointi tatu kwa mara ya pili sasa ndani ya dimba la Nangwanda Sijaona wanapokutana na Azam FC, linahitaji busara kulipokea.

Ndoto ya kocha, John Stewart Hall, huwa haiko mbali sana. Huyu ni kocha ambaye kila timu hiyo inapoyumba, hurejeshwa kuweka mambo sawa. Kuachana na Joseph Omog hayakuwa maamuzi sahihi kwa Azam FC, ni mmoja wa makocha bora kabisa ambao wangeweza kutimiza ndoto za wamiliki wa klabu hiyo.

Ni kama Real Madrid walipoamua kumtimua Carlo Ancelotti. Ni kama Louis Van Gaal alivyoamua kumuuza Angel Di Maria. Licha ya Omog kuwa kocha pekee aliyewapa Azam FC ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huyu ni kocha anayelifahamu vema soka la Afrika na tayari alishaanza kulijua sana soka la Kibongo.

Kichapo walichopata kwa mara ya pili mfululizo kutoka kwa Ndanda FC kinahitaji utulivu kukipokea, vinginevyo habari za kumrejesha kocha, John Stewart Hall, zinaweza kuibuka. Azam wanapaswa kutengeneza wachezaji na makocha watakaodumu na timu kwa muda mrefu. Kocha Zeben Hernandez anaonekana atafanikiwa hata kama si msimu huu.

Hakuna haja ya kuanza kunyoosheana vidole, ni muda wa kukusanya nguvu kuelekea mechi iliyo. Hakuna haja ya kumuota Stewart Hall, Azam FC wanahitaji kumpa mwalimu muda. Wanahitaji kupata mwalimu ambaye atadumu na kikosi angalau kwa misimu miwili.

Pesa wakati mwingine si kila kitu kwenye soka, ndiyo maana pamoja na uwekezaji mkubwa wa PSG na Manchester City, bado klabu hizo zinachechemea kunako klabu bingwa barani Ulaya. Hakuna haja ya kufanya makosa ya kumwondoa Zeben Hernandez, anapaswa kupewa usaidizi wa karibu ili aweze kujenga kikosi imara.

Hakuna timu isiyofungwa, lakini Azam wanapaswa kuhakikisha wanafanya vizuri sana hasa kwenye mechi zao za nyumbani. Msimu huu mikoani ni pagumu sana, ndiyo maana hata Yanga alipepesuka dhidi ya Ndanda FC kule Mtwara na akaanguka dhidi ya Stand United pale Shinyanga.

Katika mbio za fahari watatu, Simba tu ndiyo hawajapoteza mchezo wowote, lakini pia hawajacheza mechi hata moja nje ya Dar es Salaam. Bado Azam wanayo nafasi ya kufanya vizuri wakiwa na kocha Hernandez. Mabadiliko ya mara kwa mara ndani ya benchi la ufundi yamechangia sana kuirudisha nyuma timu ya Azam. Hakuna haja ya kumuota Stewart Hall, ni muda wa kumuunga mkono Hernandez.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -