Friday, December 4, 2020

Kichuya abeba mikoba yote Simba

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAINAB IDDY,

WINGA mpya wa Simba, Shiza Ramadhan Kichuya, hivi sasa anaonekana kuwa lulu tangu kutua kwenye kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi msimu huu.

Kichuya alijiunga na kikosi hicho kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar aliyoitumikia kwa miaka minne kwenye kikosi cha vijana kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka juzi.

Tangu aanze kuitumikia Simba katika mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara, ameweza kuifungia mabao saba kati ya 17 waliyofunga timu hiyo.

Idadi hiyo ya mabao aliyoifunga Kichuya ni kubwa kwani hakuna mwanandinga yeyote ndani ya kikosi hicho aliyeweza kuyafikia.

Pia Kichuya amepiga pasi za mwisho tano ambapo ukijumlisha na yale aliyotia nyavuni, ni kwamba Kichuya anakuwa ameshiriki katika upatikanaji wa mabao 12 katika klabu yake.

Idadi hiyo ya Kichuya ya mabao ni sawa na asilimia 71 ya mabao yote ya Simba waliofunga msimu huu na hivyo kuonekana ni moja ya wachezaji muhimu kwa miamba hiyo ya Msimbazi.

Jambo linalomfanya kuonekana kuwa muhimu katika Simba ni kutofanya makosa pindi anapopewa nafasi ya kupiga penalty, kwani hadi sasa ameshapiga mbili pasipo kukosa.

Hii ina maana kuwa, ili kuizuia Simba msimu huu isitikise nyavu zako, ni lazima uanze kumfikiria Kichuya kwanza kumzuia asifunge na wala asitoe pasi, kwani yeye ndiye ameonekana kuwa mwiba wa wapinzani wao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -