Tuesday, November 24, 2020

Guardiola majanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MANCHESTER, England

HATIMAYE Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, alijikuta akishindwa kutamba dhidi ya klabu yake ya zamani ya Barcelona.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa kocha huyo raia wa Hispania kushindwa kuibuka na ushindi katika michezo minne mfululizo.

‘Gundu’ la Guardiola lilianzia katika mtanange wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Celtic, ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 3-3.

Mchezo uliofuata wa Ligi Kuu England, matajiri hao walichezea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tottenham, kabla ya kulazimisha sare na Everton na kisha kuchapwa na Barca.

Katika mtanange huo uliochezwa juzi nchini Hispania kwenye Uwanja wa Nou Camp, Guardiola alishindwa kuizuia Barca kuibuka kidedea kwa ushindi mnono wa mabao 4-0.

Kwa upande mwingine, wengi walitegemea kuiona Man City ikiambulia kichapo katika mchezo huo na hilo lilitokana na ubora wa vikosi viwili hivyo.

Kwa maana hiyo, katika michezi minne ya mashindano yote, Guardiola, ambaye alikuwa akiinoa Bayern Munich kabla ya kutua Etihad, hajapata furaha ya ushindi.

Mchezo huo wa hatua ya makundi ulimshuhudia mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Lionel Messi, akipachika ‘hat-trick’, na ndiye aliyekuwa msumari wa moto kwa kocha wake wa zamani, Guardiola.

Ikumbukwe kuwa, matokeo hayo yamekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu Man City ilipoambulia pointi moja mbele ya Everton.

Licha ya kuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani, Man City ilitoka sare ya bao 1-1.

Ikumbukwe kuwa, akiwa na Barca na Bayern, Guardiola hakuwa katika hali mbaya kama aliyonayo hivi sasa.

Baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuliongoza benchi la ufundi la Barca, Guardiola alianza majukumu hayo kwa kupoteza mchezo wake wa kwanza wa La Liga dhidi ya Numancia.

Mchezo wake wa pili, Guardiola alipoteza akiwa nyumbani dhidi ya Racing Santander.

Matokeo hayo yalianza kumweka juu Guardiola, kwani alishinda mara 19 katika mechi 20 za ligi na zilizobaki alitoa sare, mpaka pale alipotoa sare na Real Betis.

Mchezo uliofuata, Guardiola alichezea kichapo dhidi ya Espanyol, iliyokuwa ikinolewa na Mauricio Pochettino.

Kilichofuata kwa Guardiola ni kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi tano na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza katika maisha yake ya soka.

Mechi yake ya kwanza kuiongoza Barca katika Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa dhidi ya Lyon.

Ni katika kipindi hicho ndipo alipoiongoza Barca kunyakua taji la La Liga, Copa del Rey na lile la Ulaya.

Kuanzia hapo, akiwa na Barca, Guardiola hakuwahi kuingia kwenye historia ya kucheza michezo mitatu mfululizo bila ushindi.

Akiwa Bayern, katika msimu wake wa kwanza, alicheza mechi 11 bila kupoteza na hakuwahi kupoteza mechi tatu mfululizo.

Majanga mengine ya kupoteza mechi nne mfululizo kwa Guardiola yalijitokeza mwaka jana, ambapo alifungwa mara mbili katika michezo ya Bundersliga, akafungwa na Borussia Dortmund katika mchezo wa Kombe la ligi kabla ya kulala mabao 3-0 dhidi ya Barca katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Jinamizi hilo ni kama ‘lilimfufua’ Guardiola, ambaye aliifanya Bayern kuwa tishio, hasa katika msimu wake wa mwisho klabuni hapo ambapo alishinda mechi 12 mfululizo, huku akikiwezesha kikosi hicho kunyakua taji la Bundesliga.

Kuanzia hapo, kikosi hicho cha Guardiola hakikukumbwa na balaa la kupoteza mechi mbili mfululizo.

Alipokabidhi mikoba ya kuinoa Bavarian kwa Carlo Ancelotti, Gaurdiola alikuwa na asilimia 75 za kuibuka na ushindi katika kila mchezo.

Mbali na ushindi, Guardiola aliiwezesha Bayern kucheza soka la kuvutia uwanjani.

Hivyo, kwa kucheza mechi nne bila ushindi akiwa na Man City, ni jambo lililowashitua wachambuzi wa soka na hata mashabiki wa Etihad.

Kwa mujibu wa msimamo wa ligi, Man City wako kileleni baada ya kujikusanyia pointi 19 katika michezo nane, hivyo wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Lakini pia, licha ya kipigo kutoka kwa Barca, bado Man City wana nafasi ya kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, kitendo cha kupoteza michezo minne mfululizo ni mwiba mchungu kwa Guardiola.

Wachambuzi wamedai kuwa, kwa sababu hii ni mara yake ya kwanza kukutana na balaa hilo kwa kipindi chake chote tangu alipoanza kufundisha soka, huenda hilo likawa anguko la Mhispania huyo.

Guardiola na Man City yake watashuka dimbani keshokutwa kumenyana na Southampton katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu England.

Lakini je, kiungo huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Hispania ataweza kuondosha mkosi huo au atajichimbia shimo kwa kufikisha mechi tano bila ushindi?

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -