Friday, December 4, 2020

Itafakari upya sababu yako ya kutaka kuingia katika mahusiano

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

KUMPENDA fulani haitoshi kuwa sababu madhubuti ya wewe kuingia katika mapenzi. Unaweza kumpenda na asikupende, hivyo ukiingia naye katika uhusiano ni dhahiri utakuwa huna amani wala furaha. Mapenzi ni zaidi ya kumpenda fulani na kumfuata.

Mapenzi ni zaidi ya suala la kuahidiwa maisha mazuri na ukakubali kuingia. Kuwa makini na yaangalie maisha yako kwa undani hasa. Maisha yako yanapaswa kuangaliwa kwa umakini mpana na si kwa namna ya furaha ya leo bila kuitafakari kesho yako.

Ndiyo, ni vyema kuingia katika uhusiano na mtu unayempenda ila vipi kuhusu yeye kwako? Hisia zinafanana au kwa kuwa umeona unampenda basi ukaona inafaa kuwa naye? Acha kukurupuka kisa umegundua unampenda. Unahitaji umakini, uelewa ili kuwa na ndoa ya amani na furaha. Kumpenda pekee haitoshi.

Wengi wanalia katika mapenzi kwa sababu wanapupa na mambo. Mapenzi yanapasa kukupa furaha amani na utulivu wa akili. Katika maana pana mapenzi yanapasa kukufanya hata kuwa na morali ya kweli katika kupambana na changamoto za kimaisha. Ila haya kwako hayawezekani kama uamuzi unaochukua ni wa haraka na hujajipa muda wa kutosha kutafakari mambo na mhusika kimapana.

Najua wengi wanajua kuwa kuna watu waliwaamini na kuwatenda. Wewe unajipanga vipi kabla ujaingia katika uhusiano ili usikutane na mambo hayo? Au ndiyo Mungu anajua!

Inafaa uamue uhusiano wako mwenyewe hata kabla hujakubaliana na mtu. Umsome na kumjua mwenzako. Ujiulize na kujua hasa ni kitu gani utaenda kukipata katika uhusiano wako. Kuna wengi wanaingia katika uhusiano bila kujua akili za wenzao zinawasoma na kuwaona maishani mwao ni kuwa ‘ma girlfriend/ boyfriend’ tu. Baina yao hakuna mipango madhubuti ya maisha ya baadaye.

Ndiyo maana watu wa aina hii ni miaka mingi imepita tangu wawe katika uhusiano ila hakuna suala la kuzungumzia ndoa wala mipango bora ya maisha ya baadaye. Wao wanachukuliwa kama watu wa kupita tu. Kwanini unataka kuwa katika uhusiano?

Katika uhusiano kuna raha na amani ila mpaka umpate mtu sahihi na mwafaka katika maisha yako. Na mtu wa aina hii huwezi kumpata kwa kumhukumu kwa juu juu na kwa ofa zake za bia, hapana. Unahitajika kutuliza akili na kujipanga vizuri kuweza kujua nani hasa anafaa katika maisha yako.

Kuna watu wapo tayari kukugharamia karibu kila kitu kukufanya uamini wanakupenda. Watakupa hiki na watakupeleka kila mahali unapotaka, yote kukufanya uamini kuwa wanakupenda. Ila ukweli ni kuwa ndani yao wanazuzuliwa na upya wako katika macho yao, sasa ukiacha kuwa makini unaweza kujikuta unaamini kuwa unapendwa na kujikabidhi mikononi mwao bila kujua kuwa unapotea.

Wengi mnakosea kupima upendo na thamani ya mavazi mnayonunuliwa. Wengi mnaamini kama mtu akitumia kiasi kikubwa cha pesa juu yako, basi anakupenda na kumuona fulani anayeongea na wewe pamoja na kukuahidi mambo mengine kuwa kaishiwa. Yote inawezekana ila kuwa makini ili uweze kujua ni wapi hasa unatakiwa kusimama.

Kumpenda fulani ni jambo zuri sana ila si jambo linalotakiwa kukukimbiza moja kwa moja katika uanzishaji wa uhusiano. Kupendwa pia ni jambo linalotia faraja sana ila pia si suala linalotakiwa kukukimbiza katika uhusiano ikiwa bado hujagundua mhusika ana nafasi gani katika moyo wako.

Raha ya mapenzi inapatikana pale kila mmoja anapokuwa na hisia za kweli za upendo na mwenzake. Pale kila mmoja anapoamua kumkubali mhusika kikamilifu na kujitoa kwa dhati kwa ajili yake. Hapa mapenzi yataleta amani na maana kusudiwa.

Mapenzi si suala la ‘outing’ na kubadilisha viwanja vya matumizi, hapana. Kuwa makini huku ukijua furaha yako katika mapenzi haipo kwa mtu mwenye kiwango kikubwa cha pesa au  kwa mwanamke mwenye umbo la mdoli. Furaha yako itapatikana kwa aliye na hisia za dhati juu yako na akakukubali na ukamkubali kikamilifu bila kujali sana nafasi yake kiuchumi.

Kuwa makini uamuzi wako wa leo unaweza kukupa furaha au uchungu wa kutisha katika maisha yako ya kesho. Mapenzi yatakupa amani na raha kama utakuwa na mtu mwafaka katika maisha yako. Na katu huwezi kuwa na mtu mwafaka kama unapapara katika maamuzi yako.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -