Monday, October 26, 2020

Simba, Yanga na msemo wa wengi wape

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

‘WENGI wape’ ni msemo wa Kiswahili wenye maana kubwa sana kwenye maisha ya kila siku hasa katika nchi ya kidemokrasia kama ya Tanzania.

Ndiyo maana licha ya upinzani mkubwa kutoka Ukawa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, lakini bado Rais Dk. John Magufuli, aliingia Ikulu kwa sababu wengi waliamini katika Tanzania ya Hapa Kazi Tu na si ile ya Mabadiliko.

Waswahili pia wanasema; ‘Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu’ ndiyo maana siku zote watu wengi wakiunga mkono jambo moja kamwe huwezi kupingana nao.

Lakini pia siku zote kwenye wengi lazima kuna kutofautiana, kwa sababu haiwezekani kundi la watu likaamini kwenye kitu kimoja, ndiyo maana maamuzi yoyote ya kidemokrasia huangaliwa asilimia kubwa watu inataka nini ili kufikia uamuzi.

Kundi moja kupinga uamuzi haimaanishi kuwa uamuzi fulani ni batili ndiyo maana Wazungu wanaamini katika kitu wanaita ‘Majority rule’ yaani wakimaanisha kundi lenye watu wengi ndilo lenye nguvu za kufanya maamuzi.

Kupitia imani hii ya wengi wape, labda tujiulize tu, asilimia kubwa ya wanachama wa Simba na Yanga wanataka nini? Je, wanataka mabadiliko? Au wanataka kubaki kwenye mfumo ule ule wa miaka nenda rudi? Jibu wanalo wenyewe!

Lakini kupitia mikutano mikuu kadhaa ya karibuni iwe ya dharura au rasmi katika klabu hizi mbili, nadhani tumeweza kupata picha ni kitu gani asilimia kubwa ya hawa watu wanataka.

Hivyo kwa kuheshimu msemo wa wengi wape nadhani ni busara hawa wengi wakasikilizwa kwa sababu katika nchi hii ya Tanzania ambayo tunaamini katika demokrasia tunakubaliana kitu kimoja ‘sauti ya wengi ni sauti ya Mungu’.

Lakini, wakati tukiendelea kuulizana wengi wanataka nini tayari nasikia Serikali kupitia Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Mohamed Kiganja, imepiga marufuku harakati zote za mabadiliko kwenye klabu za Simba na Yanga.

Katika taarifa ya Serikali, wameweka wazi kuwa lazima michakato hii ifuate sheria, kitu ambacho nakiunga mkono kwa asilimia 100, kwa sababu vyovyote inavyokuwa sheria za nchi ni lazima ziheshimiwe katika kila jambo.

Taarifa ile ya Serikali imeenda mbali zaidi kusema kuwa mchakato huu usimame kwa sababu eti kuna watu wanaupinga na wamepeleka malalamiko yao BMT na kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo!

Kauli hii kidogo ina ukakasi, binafsi ningeshangaa kama michakato mizima hii ya kubadili mfumo ingeenda bila kutokea na mawazo ya kupinga kwa sababu naamini kwenye wengi kutofautiana kupo.

Ndiyo maana Waswahili wanasema kuna wakati lazima ‘watu wakubali kutokukubaliana’ kwa sababu si kila kinachosemwa kinaweza kueleweka kwa kila mtu, kuna watu wana misimamo yao na pointi zao ambazo ni tofauti, lakini hilo halimaanishi wazo lingine si sahihi.

Hivyo badala ya kuzuia mchakato kwa sababu watu wanaupinga, Serikali inatakiwa kurudi kwenye ule msemo wa ‘wengi wape’ na kujiuliza asilimia kubwa ya wanachama wa Yanga na Simba wanataka nini.

Kama wengi hawataki mabadiliko basi yazuiwe, lakini kama asilimia kubwa inayataka basi yafanywe kwa sababu siku zote sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

Nitashangaa kuona maamuzi yoyote ya mchakato huu wa mabadiliko ndani ya Simba na Yanga unatolewa kuunga mkono wachache badala ya kile kinachotakwa na wengi ambao ndio wenye klabu yao.

Sitegemei kusikia mchakato huu unazuiwa kwa kigezo kuwa kama wanataka kumiliki timu basi waanzishe za kwao kama Said Salim Bakhresa aliyeanzisha klabu yake ya Azam.

Maana kila mtu ana maamuzi na fedha zake, Bakhresa ameanzisha timu yake mwenyewe kwa sababu fedha na akili yake ilimtuma kufanya hivyo, Mohamed Dewji ‘Mo’ anataka kumiliki asilimia 51 ya hisa pale Simba kwa sababu akili na fedha zake zinamtuma kufanya hivyo.

Na wote wanafanya hayo kwa sababu wana malengo yao na wasipangiwe namna ya kutumia fedha zao, waachwe wazitumie watakavyo ilimradi tu wafuate sheria na katiba ya klabu hizi wakati wakifanya hivi kama ambavyo BMT imesema.

Binafsi naamini wanachama wa Yanga na Simba ndio wenye kauli ya mwisho ya kuamua nini wafanye na klabu zao na kama wakiamua mabadiliko waachiwe wayafanye kwa sababu ndiyo wanayataka baada ya kujiendesha kwa utegemezi kwa miaka kibao.

Lakini, pia kama wakiamua kubaki kwenye mfumo wa sasa waachwe wabaki maana wenyewe ndio wenye mamlaka ya mwisho na timu yao na si mtu wala taasisi nyingine yoyote.

Cha msingi katiba za klabu na sheria za nchi zifuatwe kwenye kila kitu na kusitokee ukwamishwaji wa aina yoyote kwa sababu kufanya hivyo kunaweza kubomoa zaidi ya kujenga katika klabu hizi.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -