Saturday, October 31, 2020

Majanga haya yataimaliza Man United

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

JUZI Jumamosi, Manchester United walishindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Burnley, licha ya mchezo huo kuchezwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford.

Man United walionekana wazi kuutawala mchezo huo dhidi ya wapinzani wao lakini hakuna kilichotokea zaidi ya timu hizo kutokufungana.

Licha ya kuwakamata vilivyo vijana hao wa kocha, Sean Dyche, Man United waliambulia pointi moja.

Man United walikosa nafasi za wazi na majanga zaidi ni pale kocha wao, Jose Mourinho, alipolimwa kadi nyekundu.

Lakini pia, kiungo wao Ander Herrera ambaye amekuwa katika ubora wa hali ya juu, naye alipewa adhabu hiyo na kujikuta akimalizia mchezo akiwa nje ya uwanja. Haikuwa siku nzuri kwa Mashetani Wekundu.

Mpaka sasa, kikosi hicho kimeacha pointi nane na mahasimu wao Manchester City ambao ndio vinara wa Ligi Kuu England.

Katika michezo sita ya ligi iliyopita, Man United wameshinda mara moja pekee na hilo ni jambo linalowaumiza vichwa mashabiki wake kwa sasa.

Hata hivyo, wachambuzi wa soka wamezitaja sababu mbalimbali zinazoiua Man United, wanaamini kuwa huenda zikaendelea kukimaliza kikosi hicho katika michezo ijayo.

Kupotea kwa Ibrahimovic

Baada ya kufunga mabao manne katika michezo yake minne ya mwanzo pale Old Trafford, Zlatan Ibrahimovic amepoteza ubora wake.

Takwimu za uwanjani zinamkataa straika huyo wa kimataifa wa Sweden.

Katika mchezo dhidi ya Burnley, hakupachika bao licha ya mashuti yake 12 yaliyolenga lango.

Nyota huyo amekosa nafasi nane za wazi na hiyo ni zaidi ya mchezaji yeyote wa Ligi Kuu England tangu kuanza kwa msimu.

Akiwa kwenye ubora wake, fowadi huyo amekuwa msaada mkubwa kwa Man United na hata kupotea kwake kumeiathiri timu hiyo kwa kiasi kikubwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ibrahimovic kucheza mechi sita mfululizo bila kucheka na nyavu tangu majanga hayo yalipomtokea mwaka 2007 akiwa na Inter Milan.

Huenda Man United wakaendelea kutaabika zaidi katika michezo ijayo, ikiwa staa wao huyo ataendelea ‘kuzingua’.

Ubovu wa kikosi kizima cha Man United

Takwimu zinaonesha kuwa Man United ndiyo timu pekee iliyopoteza nafasi nyingi za mabao msimu huu kwani imefanya hivyo mara 16.

Lakini pia, wanashika nafasi ya tatu kutoka chini linapokuja suala la kupiga mashuti.

Mbali na Ibrahimovic, Wayne Rooney, Pogba na Juan Mata walikosa nafasi nyingi za mabao katika mchezo wa juzi dhidi ya Burnley.

Ukikiangalia kikosi cha sasa cha Man United, ni wazi wachezaji wake wote wamepoteza hali ya kujiamini.

Vurugu za Mourinho

Mourinho naye siku hizi amekuwa akizidiwa nguvu na tabia yake ya jazba.

Kocha huyo raia wa Ureno alionesha kukasirishwa na kitendo cha timu yake kunyimwa penalti katika mchezo wa juzi dhidi ya Burnley na kutokana na jazba zake zilisababisha alimwe kadi nyekundu.

Ukiachana na hilo, mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 53, anakabiliwa na mashtaka ya utovu wa nidhamu kutokana na  kauli zake tata alipokuwa akimzungumzia mwamuzi, Anthony Taylor, aliyechezesha mtanange dhidi ya Liverpool.

Kuna uwezekano mkubwa wa Mourinho kufungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi katika michezo ijayo na hilo litakuwa ni tatizo kwa kikosi chake.

Adhabu ya Herrera

Herrera alilimwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu kiungo wa Burnley, Dean Marney.

Man United wataikosa huduma ya Herrera katika mchezo wa mwishoni mwa wiki ijao dhidi ya Swansea.

Hilo ni pengo kwa Man United ikizingatiwa kuwa nyota huyo amekuwa sehemu muhimu ya safu ya kiungo ya timu hiyo katika siku za hivi karibuni.

Licha ya mchango wake katika ulinzi kumrahisishia kazi Pogba, hakuna mchezaji wa Man United anayemfikia Herrera kwa wastani wa pasi katika kila mchezo.

Baada ya Mourinho kusaka uwiano wa eneo la kiungo, ni Herrera ndiye aliyethibitisha kuwa anaweza kukata kiu ya Mreno huyo.

Kumkosa Herrera katika mtanange dhidi ya Swansea, ni pigo kwa Mourinho.

Wimbi la majeruhi

Kwa kipindi cha wiki moja tu, Mourinho amepoteza idadi kubwa ya mabeki wake kutokana na majeruhi.

Hakuna ubishi kuwa kukosekana kwa nyota mpya, Eric Bailly ni tatizo zaidi.

Staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, amekuwa sehemu muhimu ya safu ya ulinzi tangu alipotua Old Trafford akitokea Villarreal.

Majeraha ya goti aliyoyapata katika mchezo dhidi ya Chelsea ambapo Man United ilichapwa mabao 4-0, yatamweka nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua miezi miwili.

Lakini pia, ‘pacha’ wake Chris Smalling naye ni majeruhi na imeelezwa kuwa alicheza dhidi ya Chelsea akiwa na maumivu. Wawili hao wanaungana na beki wa kulia, Antonio Valencia.

“Ni wachezaji watatu ambao walikuwa wakianza katika kila mchezo na sasa tumewapoteza kwa wakati mmoja,” alisema Mourinho.

Kuwakosa mastaa hao ni majanga kwa Mourinho ambaye sasa atalazimika kuwaamini Marcos Rojo na Matteo Darmian katika ulinzi wa kati.

Ni wazi huo ni mtihani mzito hasa ikizingatiwa kuwa Man United watavaana na Arsenal, West Ham na Everton katika michezo ijayo ya Ligi Kuu England.

Kukosekana kwa Mkhitaryan

Hakuna asiyetambua uwezo wa Henrikh Mkhitaryan. Katika msimu wake wa mwisho pale Borussia Dortmund kabla ya kutua Old Trafford, alikuwa amefunga mabao 23 na ‘asisti’ 20.

Amekosa namba ya uhakika chini ya Mourinho na hakupata hata nafasi ya kukaa benchi katika mchezo dhidi ya Burnley.

Kuelekea mechi hiyo, Mourinho alikiri wazi kuwa Mkhitaryan hakuwa majeruhi.

Alichosema Mreno huyo ni kwamba Mkhitaryan anaendelea kutazama kwa ukaribu kwa sababu hajazoea soka la England.

Mourinho alisema nyota huyo anahitaji muda lakini ukweli ni kwamba hicho sicho kilichoifanya Man United kutoa pauni milioni 26 kumsajili.

Mbali na ligi, Mkhitaryan amekosa nafasi hata kwenye mechi za Kombe la Ligi (EFL Cup).

Kutokana na wimbi la majeruhi, huenda sasa ukawa ni wakati wa Mourinho kuanza kumtumia staa huyo raia wa Almenia.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -